
Blog yenu ya Easymen leo ilipata bahati ya kutembelea ofisi za Taasisi ya Kutangaza na Kukuza Utaalii katika Mkoa wa Tanga ijulikanayo kama Tanga Tourism Network Association (TATONA).Ofisi za Taasisi hii zipo katika Jengo la Sachak House mkabala na Posta kuu ya Tanga au karibu kabisa na Mahakama ya Mwanzo.


Mimi nikishow love na Laurent (mwenye shati la blue) ambaye ni katibu wa Taasisi hiyo ya TATONA.

Ofisi ya TATONA

Laurent Akiwa Ofisini akila mzigo.

Kwa mujibu wa Laurent ameiambia blog hii kuwa Taasisi hiyo ipo katika hatua za mwisho kabis za kuanzisha Website yake ili kurahisisha upatikanaji wa Taarifa za Utalii.
Pia allidokeza blog hii kwamba wako katika Maandalizi ya Kwenda Arusha katika Maonyesho ya Utalii yajulikanayo kama KARIBU FAIR yatakayoanza tarehe 2 hadi 6 June 2010.
No comments:
Post a Comment