SIKILIZA NYIMBO ZA EASYMEN HAPA:


Electronic Press Kit
Quantcast

Tazama Small Interview ya Easymen Studio Hapa:

Thursday, August 2, 2012

BRIDER KHAN, KICHWA KINACHOWAKILISHA TANGA KWENYE FIESTA SUPER NYOTA. MUWEZESHE AWE MSHINDI KWA KUMPIGIA KURA !!

Ili Kuweza kumpigia kura BRIDER KHAN awe mshindi kwenye shindano la Fiesta Super Nyota, Andika Neno FIESTA acha nafasi andika namba yake ya ushiriki ambayo ni kisha tuma kwenda namba 15678. Hapo utakuwa umemuwezesha yeye na Mkoa wetu wa Tanga kuibuka na ushindi.
Kila ujumbe wa kumpigia kura utatozwa Tsh 49 tu.

Sunday, June 3, 2012

KITUO CHA VIJANA NGUVUMALI TANGA CHAPOKEA WANACHAMA WAPYA 10 KUJIUNGA NA KITUO HICHO!


Baadhi ya wanachama wapya waliokuja kujiunga na kituo cha vijana nguvumali Tarehe 02/06/2012

Wanachama wapya katika picha.

Wanachama wapya wa kituo cha vijana nguvumali,Tanga.wakiwa katika picha baada ya mazungumzo na Uongozi wa kituo kwa kupewa historia fupi ya Kituo na kukaribishwa kituoni siku ya Jumamosi 02/06/2012.

Thursday, December 22, 2011

BAADHI YA PICHA ZA MATUKIO YA ATHARI ZA MAFURIKO KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM!!






Blog hii ya Easymen inatoa pole kwa waathirika wote waliokumbwa na maafa hayo.na pia tunamuomba mwenyezi Mungu azilaze pema peponi roho za marehemu wote waliopoteza maisha kwa ajili ya mafuriko hayo. Tuko nanyi katika kipindi hiki kigumu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA. AMEN.

Wednesday, December 14, 2011

MWISHO NA MERYL WAFUNGA NDOA RASMI NCHINI NAMIBIA.!!!


Ilikuwa siku ya kupendeza kabisa kwa ndugu Mwisho Mwampamba na Mwanadada Merly kutoka Namibia kufunga pingu za maisha nikimaanisha ndoa na kuitwa mume na mke. Ndoa hii ilifungwa tarehe 10 mwezi huu wa 12 pande za Parliament Gardens Windhoek Namibia.




Blog hii ya Easy Men inawatakia maisha mema katika ndoa yenu pamoja na malezi mema ya mtoto wenu mliompa jina la Monkey.

Friday, December 2, 2011

BURIANI ABBEL MOTIKA, ( MR EBBO) MUNGU AILAZE ROHO YAKO MAHALA PEMA PEPONI.



Ni ngumu kuamini kama rafiki na kaka yetu mpendwa Abbel Motika umetutoka duniani. lakini ukweli ni kwamba kweli Mr Ebbo ametutoka duniani.
Leo asubuhi saa 12 asubuhi nilipata simu kwamba Mr Ebbo amefariki dunia.sikuweza kuamini hadi nilipoamua kufunga safari milango ya saa 4 asubuhi nyumbani kwa wazazi wake maeneo ya Kisosora jijini Tanga, Nilipofika nyumbani kwa Mzee Motika ambaye ndie baba mzazi wa Mr Ebbo nilianza kuamini baada ya kuona watu wengi kidogo na magari na pikipiki. nilijitahidi kumpata baba mzazi wa Mr Ebbo mzee Motika na akanihakikishia kweli mwanae Abbel Motika maarufu kama Mr Ebbo ambaye amewahi kuwika katika tasnia ya Muziki wa bongofleva na vibao mbalimbali kama Mimi Mmasai na Kamongo kwamba amefariki dunia jana alfajiri jijini Arusha alikokuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda kidogo.
Kuhusu taratibu za mazishi Mzee Motika alinieleza kwamba Mazishi ya mtoto wake Abbel Motika maarufu kama Mr Ebbo yatafanyika jijini Arusha siku ya Jumatatu na msiba utakuwa nyumbani kwao Arusha karibu na Club Masai Camp. Misa ya kumombea marehemu itaanza Jumatatu saa 7 mchana.
Pia nilibahatika kuongea na marafiki wenzangu ambao Mr Ebbo alikuwa rafiki yetu wa karibu kama, Jeff maarufu kama Jeff Production, Msanii wa bongofleva Ruwa,na Ben Naburi nao walionyeshwa kushtushwa na taarifa hizi kwa sababu hali ya ugonjwa wa Mr Ebbo haikuwa siriasi kiasi hicho,
Kutoka kwa marafiki wa jijini Tanga, taratibu za kusafiri kwenda kwenye mazishi ya kijana mpendwa wetu zimeandaliwa na marafiki wote wanaohitaji kwenda kwenye msiba huu wafike nyumbani kwa wazazi wa Mr Ebbo au wawasiliane na Jeff Production au Ben Naburi. safari ya kuelekea kwenye msiba kwa marafiki wa marehemu itafanyika siku ya Jumatatu saa 10 alfajiri ili kuwahi misa inayotazamiwa kuanza majira ya saa 7 mchana jijini Arusha.
Blog hii ya Easymen inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote bila kuwasahau mashabiki zake wote wa muziki wake kokote walipo duniani. Mungu ilaze roho ya marehemu Abbel Roshoroo Motika mahala pema peponi

AMINA.

Sunday, November 6, 2011

WADAU SAMAHANI KWA KUWA KIMYA KWA MUDA MREFU,SASA NIMERUDI NA NEWS ZITAKUJA KAMA KAWAIDA, NAWAPENDA NYOTE NA NAWATAKIA SIKUU NJEMA YA EIDD !!!


Kidogo Jamani tushee kapicha haka angalau munione na mimi sikukuu yangu nilikula vipi. Hapa nikiwa na rafiki yangu na Producer wangu maarufu kama Danny.(Mwenye miwani)

Saturday, September 10, 2011

BREAKING NEWS:KUZAMA KWA MELI YA MV SPICE ISLANDERS !!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUZAMA KWA MELI YA SPICE ISLANDERS
Usiku wa kuamkia leo tarehe 10/09/2011,majira ya saa 9 za usiku kumetokea ajali ya kuzama kwa meli ya MV SPICE ISLANDERS katika bahari ya eneo la Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja.
Taarifa ya Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa Rais,Mohamed Aboud Mohamed imesema Meli hiyo ilikuwa ikitokea Unguja kuelekea Wete mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo meli hiyo ilikuwa imepakia Abiria pamoja na Mizigo.
Waziri Aboud amesema Serikali bado inaendelea na jitihada za kukitafuta chombo hicho pamoja na watu waliokuwemo.
Amesema kwamba Serikali tayari imeshatuma vyombo vya Uokozi,Ulinzi na Usalama na mtakuwa mkipewa taarifa mara kwa mara.
Waziri Aboud amewataka wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu na tuendelee kusikiliza taarifa za Serikali kupitia vyombo vya habari ili kupata taarifa zaidi.

IMETOLEWA NA ;
IDARA YA HABARI (MAELEZO) ZANZIBAR
10/09/2011

Sunday, August 21, 2011

RAISI DKT,JAKAYA KIKWETE AKAGUA CHANZO CHA MAJI MJI WA LINDI !!!


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akikagua chanzo cha maji ya Minispaa ya Lindi kilichopo Kitunda kata ya Msinjahili manispaa hiyo leo mchana kwenye siku ya pili ya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Lindi(picha na Freddy Maro).

TUNAWASHUKURU SANA WANA AFRIKA MASHARIKI !!!


Again, Ahsante Kwa Support Yenu...MwanaFA&AY-Habari Ndio Hiyo Imeshinda Wimbo Bora Wa Ushirikiano Kwenye Tunzo Za Africa Mashariki EMAS...Kwa Niaba,Nashukuru Sana,Tuendelee Kuwa Pamoja..Bless!!

Saturday, June 11, 2011

VIONGOZI WA SERIKALI YA KATA YA NGUVUMALI PAMOJA NA WAZAZI WABARIKI ZIARA YA VIJANA 10 WA KITUO CHA VIJANA NGUVUMALI KWENDA NCHINI HUNGARY !!!


Leo katika ofisi zetu za kituo cha vijana Nguvumali tulifanya mkutano uliowahusisha wazazi wenye watoto amabo ni wanachama wa kituo,vijana wenyewe na Uongozi wa kata ya Nguvumali ambapo kituo hiki cha vijana Nguvumali kipo.Lengo na madhumuni ya mkutano huu ni kuweza kufahamiana wazazi na viongozi wa kituo na serikali,pia kupokea taarifa ya Kituo na viongozi pamoja na wazazi kutoa nasaha zao kwa vijana wa kituo hiki ambao watashiriki katika ziara ya kubadilishana uzoefu Itakayofanyika tarehe 15/06/2011 ambapo vijana 5 kutoka kituo hiki watasafiri kwenda nchini Hungary kwa muda wa mwezi mmoja kufanya shughuli za kujitolea na kituo kingine cha vijana kilichopo nchini humo.group lingine la vijana 5 litasafiri tarehe 25/07/2011 nalo pia litakaa nchini Hunagry kwa muda wa mwezi 1.Pichani ni meza Kuu,toka kushoto ni Afisa maendelo ya jamii kata ya Nguvumali,Mtendaji kata wa Nguvumali,Meneja wa kituo,Mh Diwani wa kata ya Nguvumali na Katibu wa kituo.

Wazazi pamoja na wageni waalikwa wakisiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Mh Diwani wa kata ya nguvumali aliyoitoa katika mkutano huo.

Wazazi upande wa kinamama wakisikiliza kwa makini.


Wazazi pamoja na vijana wao ambao ni wanachama wa kituo hiki wakisiliza kwa makini wakati mkutano huu ukiendelea leo katika kituo cha vijana Nguvumali.

Mimi Pashua nikipokea Hati ya Bima ya Afya ya Kimataifa toka kwa mgeni rasmi ambaye ni Mh Diwani wa Kata ya Nguvumali ambayo itanisaidia kama nitapata matatizo ya kiafya kwa kipindi chote cha mwezi 1 nitakachokaa nchi Hungary.

Kijana John Omary akipokea hati ya bima ya afya toka kwa mgeni rasmi.

Katibu wa kituo Kassam Kassimila akipokea hati ya bima ya Afya toka kwa mgeni ambapo yeye ni miongoni mwa vijana 10 watakaoshiriki katika safari hiyo.

Kijana Linus Lucian ambaye pia ni mkuu wa nidhamu wa kituo akipokea hati ya bima ya toka kwa mgeni rasmi.

MWIZI APONEA CHUPUCHUPU KUUAWA NA WANANCHI BAADA YA KUIBA VIATU MSIKITINI !!!

Umati wa watu ukiwa umezingira msikiti wa Mabawa kungojea mwizi aliyekatwa msikitini hapo akiiba Makobazi.Uongozi wa msikiti huo ilibidi kumficha mwizi huyo ndani kutokana na wananchi wenye hasira kali kutaka kumpiga hadi kumuua.baada ya mvutano mkali kati ya wananchi waliotaka mwizi huyo atolewe ili wamuadhibu uongozi wa msikiti uliliarif jeshi la polisi ili kuleta ulinzi na kumuondoa mwizi huyo akiwa salama.mara ya kwanza walifika polisi 4 ambao pia wananchi waliwazidi nguvu jeshi la polisi lilileta kikosi cha kutuliza ghasia FFU ambapo walifanikiwa kuwadhibiti wananchi na kumtoa mwizi huyo kutoka kwenye msikiti na kumpeleka Kituoni.


Gari la polisi kikosi cha kutuliza ghasia likiondoka katika msikiti huo maeneo ya Mabawa na mwizi huyo akiwa ndani ya gari hilo.


Gari hilo la polisi likitokomea na wananchi wasijue wafanye nini.