SIKILIZA NYIMBO ZA EASYMEN HAPA:


Electronic Press Kit
Quantcast

Tazama Small Interview ya Easymen Studio Hapa:

Saturday, November 27, 2010

MWALIKO WA SHEREHE ZA UHURU WA TANZANIA NCHINI NORWAY!!!


WATANZANI WAISHIO BERGEN NORWAY TUNAFUNGUA UMOJA WETU WA WATANZANIA HAPA BERGEN NA PAMOJA NA KUSHEHEREKEA SIKU YA UHURU WA TANZANIA KWA PAMAMOJA NA WATANZANIA WENZETU POPOTE WALIPO DUNIANI SIKU YA TAREHE 10.12.2010.

KATIKA SHUGHULI YETU HII MGENI RASMI ATAKUA NI MWAKILISHI WA BALOZI WA TANZANIA KUTOKA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI SWEEDEN. TUNAWAKARISHA WATANZANIA WOTE WAISHIO BERGEN NORWAY NA NJE YA NCHI YA NORWAY KUJA KUJUMUIKA NASI KATIKA GHAFLA HII. NAWE UKIWA MMOJA WAPO KARIBU SAANA.

NAPIA TUNA PAGE YETU YA CHAMA KWENYE FACEBOOK INATAMBULIKA KWA JINA LA (WATANZANIA BERGEN) WATU WOTE WANAKARIBISHWA KUWA NA URAFIKI NASI, NA PIA TUNAKARIBISHA MAONI KWA KUPITIA ANUANU PEPE YA CHAMA NAYO NI ( WATANZANIA.BERGEN@GMAIL.COM)

UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.


KARIBUNI

Saturday, November 20, 2010

MDAU IDD AKISHOW LOVE NDANI YA BLOG !!!


Mdau wa Blog hii Ndg Idd ambaye anapatikana maeneo ya Hotnet street Tanga ,akishow love ndani ya Pozi la ukweli.

RAIS KIKWETE ASAKATA RHUMBA NA LYATONGA MREMA !!


JK akicheza na Mwenyekiti wa TLP na Mbunge wa Vunjo Mh. Augustine Lyatonga Mrema wakati wa mnuso wa kuwapongeza wabunge kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma. Kulia ni Mzee Yusuf ambaye kundi lake la Jahazi Modern Taarab lilikuwa likitumbuiza.
Picha na mdau Freddy Maro.

Wednesday, November 3, 2010

SAMWEL SITTA ACHUKUA TENA FOMU KUTETEA KITI CHAKE CHA USPIKA BUNGE LIJALO !!!


Spika anayemaliza mda wake Mhe. Samuel Sitta leo amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika wa Bunge katika Bunge la Kumi kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema wiki ijayo mjini Dodoma.


Spika Sitta amechukua fomu hiyo kupitia chama chake cha CCM katika ofisi ndogo za CCM Lumumba, Dar es Salaam na kuijaza kisha kuirudisha leo hii baada ya kukamilisha mahitaji yote ikiwa ni pamoja na kugharamia fomu hiyo kwa kiasi cha Tsh 500,000/= kwa mujibu wa taratibu wa chama hicho.


kwa Mujibu wa ibara ya 84 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, chama chochote cha siasa kilichosajiliwa kina haki ya kushiriki katika Uchaguzi wa Spika kwa kumpendekeza mwananchama wake mmoja ambaye ni Mbunge au asiye Mbunge mwenye sifa za kuwa Mbunge kuwa Mgombea wa nafasi hiyo.Katika picha juu Spika anayemaliza muda wake Mhe. Samuel Sitta akisaini kitabu cha watu waliochukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika kwenye Ofisi za CCM Lumumba.

RAIS MPYA WA ZANZIBAR DR SHEIN ALA KIAPO TAYARI KUONGOZA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA !!!


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Dk Ali Mohammed Shein Akila Kiapo cha kuwa Rais wa awamu ya saba wa Zanzibar katika sherehe zilizofanyika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja leo.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Dk Ali Mohammd Shein, akikagua gwaride rasmi la vikosi vya ulinzi katika sherhe maalum cha kua kiapo cha kuwa Rais wa Awamu ya saba wa Zanzibar, katika uwanja wa Amaan Studiam, Mjini Unguja leo.

Tuesday, November 2, 2010

MWANAMUZIKI MR II (SUGU) SASA NI MHESHIMIWA JOSEPH MBILINYI !!!!


Mwanamuziki mkongwe na muanzilishi wa muziki wa Kizazi kipya maarufu kama Bongofleva nchini Tanzania MR II maarufu kama Sugu ameweza kushinda kwa kishindo nafasi ya Ubunge kwa jimbo la Mbeya Mjini kwa Tiketi ya Chama cha CHEDEMA.Mr II au Sugu amewashukuru watanzania hususani wakazi wa Mbeya Mjini kwa imani walioionyesha kwake kwa kumchagua kwa ushindi mkubwa kuwa mbunge wao kwa kipindi cha miaka 5 ijayo.Katika shukrani zake Sugu amewaahidi wakazi wa Mbeya mabadiliko ya ukweli ya kuleta maendeleo katika Jimbo hilo.

MRISHO MPOTO ASEMA WASANII WA TANZANIA WANA ULIMBUKENI WA KUIGA UTAMADUNI WA MAGHARIBI KWA KILA KITU !!!!


Mrisho Mpoto

Msanii mahiri wa mashairi nchini,Mrisho Mpoto ameeleza kile anachoamini kwamba,tasnia ya sanaa na wasanii wa Bongo hawawezi kamwe kupata mafanikio katika ngazi ya kimataifa kutokana na ulimbukeni wa kuiga sanaa za watu wengine, kudharau asili yao na kujipachika usupastaa wa kubumba.

Mpoto aliyasema hayo wakati akiwasilisha mada yake iliyohusu Muziki wa Asili na Mashairi kwenye Jukwaa la Sanaa Jumatatu hii ambapo alisisitiza kwamba,wasanii wa bongo wamekuwa ni wa kulalama na kulia njaa kutokana na kazi wanazozalisha kushindwa kabisa kupata mvuto wa kimataifa na kushindana kwani zimekuwa kwa asilimia kubwa zikifanana na tamaduni za nje hivyo kukosa jipya.

Akijitolea mfano yeye mwenyewe Mpoto alisema kwamba, ameweza kukaa chini na kubuni sanaa ya asili ya Tanzania ambapo amekuwa akighani mashairi na kuyaweka kwenye mdundo wa muziki na hivyo kupendwa na idadi kubwa ya watanzania na kupenya kimataifa hivyo kumfanya kupata mialiko na fursa nyingi za fedha ambazo zimekuwa zikimpatia mafanikio makubwa.

Kwake yeye Mpoto anaamini kwamba, Sanaa ya Tanzania na wasanii wake hawaonekani kugundua siri ya kufanya kazi za sanaa zenye asili yao na badala yake wamekuwa makasuku wa kujifananisha na kuishi maisha kama ya Ulaya na Marekani huku kazi zao zikifanana kila kitu na hizo za nje hali ambayo imeifanya sanaa kupwaya na wasanii wenyewe kuishi maisha ya njaa.

Aliongeza kwamba, ni ngumu kupata msanii wa bongo anayefanya sanaa peke yake kwani mara nyingi lazima wachanganye na shughuli zingine ili kupata kipato kutokana na kazi zao kutowalipa.Katika hili Mpoto anaamini kwa kiasi kikubwa limesababishwa na wasanii wenyewe kukosa ubunifu, kuiga kila kitu kutoka nje, kulewa sifa za mapema, kukumbatia sanaa zisizo za asili yao na kujipachika usupastaa wa kubumba.

“Nimekuwa nikipata mialiko mingi nje ya nchi,siku chache zijazo nitaenda Denmark,Finland,Ufaransa, na Uholanzi.Si kwa kuwa napendwa sana bali ni aina ya sanaa ninayofanya ina asili yangu ya Tanzania na inanitambulisha kila ninakokwenda.Waache wasanii wengine wavae nguo chini ya makalio yao au hata watembee uchi mimi nitabaki na magunia yangu.Hili ndilo naamini litaweza kunipa mafanikio na ninayapata” alisisitiza Mpoto.

Mpoto ambaye kwa sasa ni msanii pekee aliyepata mafanikio makubwa kutokana na kupata mikataba mingi ya matangazo, mauzo ya kazi zake na mialiko ya kimataifa kutokana na kukumbatia sanaa ya asili aliwashauri wasanii wa bongo kuacha kunakiri (kukopi) sanaa za nje na badala yake wakune vichwa katika kubeba sanaa ya asili ambayo hapana shaka itawatambulisha kimataifa na kuwapa mikataba minono ya ndani na ya nje.

Mpoto aliyekuwa ameambatana na muimbaji wake wa Mjomba Band,Ismail alisema kwamba, inatia aibu na kinyaa unapoangalia sanaa za bongo kwani zinaonekana kuandaliwa na watu wenye njaa, wanaosaka fedha za fastafasta kuliko kujali nini wanapeleka sokoni hali ambayo imekuwa ikiwafanya wasanii wa Tanzania waonekane ni wa hovyohovyo, wa kudharaulika na wasio na mkakati wa kufikia mafanikio ya kisanaa.

“Kuna watu wamefanya sanaa miaka nenda miaka rudi lakini hawapigi hatua.Wamekuwa ni watu wa kulalamika bila kuzingatia ni kwa kiwango gani sanaa zao zina ubunifu na kubeba asili na utambulisho wao.Ndugu zangu tusipozingatia haya mafaniko tutayasikia tu na tutakuwa watu wa kuganga njaa na kupiga mizinga ya vocha” alimalizia Mpoto