SIKILIZA NYIMBO ZA EASYMEN HAPA:


Electronic Press Kit
Quantcast

Tazama Small Interview ya Easymen Studio Hapa:

Thursday, December 22, 2011

BAADHI YA PICHA ZA MATUKIO YA ATHARI ZA MAFURIKO KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM!!






Blog hii ya Easymen inatoa pole kwa waathirika wote waliokumbwa na maafa hayo.na pia tunamuomba mwenyezi Mungu azilaze pema peponi roho za marehemu wote waliopoteza maisha kwa ajili ya mafuriko hayo. Tuko nanyi katika kipindi hiki kigumu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA. AMEN.

Wednesday, December 14, 2011

MWISHO NA MERYL WAFUNGA NDOA RASMI NCHINI NAMIBIA.!!!


Ilikuwa siku ya kupendeza kabisa kwa ndugu Mwisho Mwampamba na Mwanadada Merly kutoka Namibia kufunga pingu za maisha nikimaanisha ndoa na kuitwa mume na mke. Ndoa hii ilifungwa tarehe 10 mwezi huu wa 12 pande za Parliament Gardens Windhoek Namibia.




Blog hii ya Easy Men inawatakia maisha mema katika ndoa yenu pamoja na malezi mema ya mtoto wenu mliompa jina la Monkey.

Friday, December 2, 2011

BURIANI ABBEL MOTIKA, ( MR EBBO) MUNGU AILAZE ROHO YAKO MAHALA PEMA PEPONI.



Ni ngumu kuamini kama rafiki na kaka yetu mpendwa Abbel Motika umetutoka duniani. lakini ukweli ni kwamba kweli Mr Ebbo ametutoka duniani.
Leo asubuhi saa 12 asubuhi nilipata simu kwamba Mr Ebbo amefariki dunia.sikuweza kuamini hadi nilipoamua kufunga safari milango ya saa 4 asubuhi nyumbani kwa wazazi wake maeneo ya Kisosora jijini Tanga, Nilipofika nyumbani kwa Mzee Motika ambaye ndie baba mzazi wa Mr Ebbo nilianza kuamini baada ya kuona watu wengi kidogo na magari na pikipiki. nilijitahidi kumpata baba mzazi wa Mr Ebbo mzee Motika na akanihakikishia kweli mwanae Abbel Motika maarufu kama Mr Ebbo ambaye amewahi kuwika katika tasnia ya Muziki wa bongofleva na vibao mbalimbali kama Mimi Mmasai na Kamongo kwamba amefariki dunia jana alfajiri jijini Arusha alikokuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda kidogo.
Kuhusu taratibu za mazishi Mzee Motika alinieleza kwamba Mazishi ya mtoto wake Abbel Motika maarufu kama Mr Ebbo yatafanyika jijini Arusha siku ya Jumatatu na msiba utakuwa nyumbani kwao Arusha karibu na Club Masai Camp. Misa ya kumombea marehemu itaanza Jumatatu saa 7 mchana.
Pia nilibahatika kuongea na marafiki wenzangu ambao Mr Ebbo alikuwa rafiki yetu wa karibu kama, Jeff maarufu kama Jeff Production, Msanii wa bongofleva Ruwa,na Ben Naburi nao walionyeshwa kushtushwa na taarifa hizi kwa sababu hali ya ugonjwa wa Mr Ebbo haikuwa siriasi kiasi hicho,
Kutoka kwa marafiki wa jijini Tanga, taratibu za kusafiri kwenda kwenye mazishi ya kijana mpendwa wetu zimeandaliwa na marafiki wote wanaohitaji kwenda kwenye msiba huu wafike nyumbani kwa wazazi wa Mr Ebbo au wawasiliane na Jeff Production au Ben Naburi. safari ya kuelekea kwenye msiba kwa marafiki wa marehemu itafanyika siku ya Jumatatu saa 10 alfajiri ili kuwahi misa inayotazamiwa kuanza majira ya saa 7 mchana jijini Arusha.
Blog hii ya Easymen inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote bila kuwasahau mashabiki zake wote wa muziki wake kokote walipo duniani. Mungu ilaze roho ya marehemu Abbel Roshoroo Motika mahala pema peponi

AMINA.

Sunday, November 6, 2011

WADAU SAMAHANI KWA KUWA KIMYA KWA MUDA MREFU,SASA NIMERUDI NA NEWS ZITAKUJA KAMA KAWAIDA, NAWAPENDA NYOTE NA NAWATAKIA SIKUU NJEMA YA EIDD !!!


Kidogo Jamani tushee kapicha haka angalau munione na mimi sikukuu yangu nilikula vipi. Hapa nikiwa na rafiki yangu na Producer wangu maarufu kama Danny.(Mwenye miwani)

Saturday, September 10, 2011

BREAKING NEWS:KUZAMA KWA MELI YA MV SPICE ISLANDERS !!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUZAMA KWA MELI YA SPICE ISLANDERS
Usiku wa kuamkia leo tarehe 10/09/2011,majira ya saa 9 za usiku kumetokea ajali ya kuzama kwa meli ya MV SPICE ISLANDERS katika bahari ya eneo la Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja.
Taarifa ya Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa Rais,Mohamed Aboud Mohamed imesema Meli hiyo ilikuwa ikitokea Unguja kuelekea Wete mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo meli hiyo ilikuwa imepakia Abiria pamoja na Mizigo.
Waziri Aboud amesema Serikali bado inaendelea na jitihada za kukitafuta chombo hicho pamoja na watu waliokuwemo.
Amesema kwamba Serikali tayari imeshatuma vyombo vya Uokozi,Ulinzi na Usalama na mtakuwa mkipewa taarifa mara kwa mara.
Waziri Aboud amewataka wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu na tuendelee kusikiliza taarifa za Serikali kupitia vyombo vya habari ili kupata taarifa zaidi.

IMETOLEWA NA ;
IDARA YA HABARI (MAELEZO) ZANZIBAR
10/09/2011

Sunday, August 21, 2011

RAISI DKT,JAKAYA KIKWETE AKAGUA CHANZO CHA MAJI MJI WA LINDI !!!


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akikagua chanzo cha maji ya Minispaa ya Lindi kilichopo Kitunda kata ya Msinjahili manispaa hiyo leo mchana kwenye siku ya pili ya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Lindi(picha na Freddy Maro).

TUNAWASHUKURU SANA WANA AFRIKA MASHARIKI !!!


Again, Ahsante Kwa Support Yenu...MwanaFA&AY-Habari Ndio Hiyo Imeshinda Wimbo Bora Wa Ushirikiano Kwenye Tunzo Za Africa Mashariki EMAS...Kwa Niaba,Nashukuru Sana,Tuendelee Kuwa Pamoja..Bless!!

Saturday, June 11, 2011

VIONGOZI WA SERIKALI YA KATA YA NGUVUMALI PAMOJA NA WAZAZI WABARIKI ZIARA YA VIJANA 10 WA KITUO CHA VIJANA NGUVUMALI KWENDA NCHINI HUNGARY !!!


Leo katika ofisi zetu za kituo cha vijana Nguvumali tulifanya mkutano uliowahusisha wazazi wenye watoto amabo ni wanachama wa kituo,vijana wenyewe na Uongozi wa kata ya Nguvumali ambapo kituo hiki cha vijana Nguvumali kipo.Lengo na madhumuni ya mkutano huu ni kuweza kufahamiana wazazi na viongozi wa kituo na serikali,pia kupokea taarifa ya Kituo na viongozi pamoja na wazazi kutoa nasaha zao kwa vijana wa kituo hiki ambao watashiriki katika ziara ya kubadilishana uzoefu Itakayofanyika tarehe 15/06/2011 ambapo vijana 5 kutoka kituo hiki watasafiri kwenda nchini Hungary kwa muda wa mwezi mmoja kufanya shughuli za kujitolea na kituo kingine cha vijana kilichopo nchini humo.group lingine la vijana 5 litasafiri tarehe 25/07/2011 nalo pia litakaa nchini Hunagry kwa muda wa mwezi 1.Pichani ni meza Kuu,toka kushoto ni Afisa maendelo ya jamii kata ya Nguvumali,Mtendaji kata wa Nguvumali,Meneja wa kituo,Mh Diwani wa kata ya Nguvumali na Katibu wa kituo.

Wazazi pamoja na wageni waalikwa wakisiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Mh Diwani wa kata ya nguvumali aliyoitoa katika mkutano huo.

Wazazi upande wa kinamama wakisikiliza kwa makini.


Wazazi pamoja na vijana wao ambao ni wanachama wa kituo hiki wakisiliza kwa makini wakati mkutano huu ukiendelea leo katika kituo cha vijana Nguvumali.

Mimi Pashua nikipokea Hati ya Bima ya Afya ya Kimataifa toka kwa mgeni rasmi ambaye ni Mh Diwani wa Kata ya Nguvumali ambayo itanisaidia kama nitapata matatizo ya kiafya kwa kipindi chote cha mwezi 1 nitakachokaa nchi Hungary.

Kijana John Omary akipokea hati ya bima ya afya toka kwa mgeni rasmi.

Katibu wa kituo Kassam Kassimila akipokea hati ya bima ya Afya toka kwa mgeni ambapo yeye ni miongoni mwa vijana 10 watakaoshiriki katika safari hiyo.

Kijana Linus Lucian ambaye pia ni mkuu wa nidhamu wa kituo akipokea hati ya bima ya toka kwa mgeni rasmi.

MWIZI APONEA CHUPUCHUPU KUUAWA NA WANANCHI BAADA YA KUIBA VIATU MSIKITINI !!!

Umati wa watu ukiwa umezingira msikiti wa Mabawa kungojea mwizi aliyekatwa msikitini hapo akiiba Makobazi.Uongozi wa msikiti huo ilibidi kumficha mwizi huyo ndani kutokana na wananchi wenye hasira kali kutaka kumpiga hadi kumuua.baada ya mvutano mkali kati ya wananchi waliotaka mwizi huyo atolewe ili wamuadhibu uongozi wa msikiti uliliarif jeshi la polisi ili kuleta ulinzi na kumuondoa mwizi huyo akiwa salama.mara ya kwanza walifika polisi 4 ambao pia wananchi waliwazidi nguvu jeshi la polisi lilileta kikosi cha kutuliza ghasia FFU ambapo walifanikiwa kuwadhibiti wananchi na kumtoa mwizi huyo kutoka kwenye msikiti na kumpeleka Kituoni.


Gari la polisi kikosi cha kutuliza ghasia likiondoka katika msikiti huo maeneo ya Mabawa na mwizi huyo akiwa ndani ya gari hilo.


Gari hilo la polisi likitokomea na wananchi wasijue wafanye nini.

SIKU TULIPOMUAGA MFANYAKAZI MWENZETU OFISINI KWA KUWA ANAKWENDA KUENDELEA NA MASOMO !!!


Mfanyakazi mwenzetu kazini aliyevaa Kitenge akipata iliyondaliwa maalum kwa ajili ya kumuaga kwa kuwa anakwenda kuendelea na masomo yake ya juu.ilikuwa ni siku ya huzuni sana kwani tulimzoea sana.


Pichani keki hiyo yenye maneno ya kwamba KILA LA HERI SHAMSA.


Pichani mkurugenzi wetu mama Ruth akimpa Zawadi ya kitenge chenye nembo ya kampuni yetu kama ukumbusho kwa mema aliyoyatenda kwenye kampuni.
Hapa mimi Pashua niliombwa kuburudisha wafanyakazi wenzangu kwenye Party hii ya kumuaga mwenzetu kwa kuimba wimbo niliomshirikisha mfanyakazi mwenzangu pia pichani anaitwa Mocky wimbo unaitwa UNFORGETABLE.

Zoezi la Kuburudisha likiendelea.


Sunday, May 22, 2011

RAISI JAKAYA MRISHO KIKWETE AHANI MISIBA YA SHEIKH YAHYA NA MZEE ATHUMANI MWINJUMA LEO !!


Rais Kikwete akipokewa na Hassan Yahya Hussein, Mtoto mkubwa wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein alipokwenda kuhani msiba wa mnajimu huyo maarufuf nyumbani kwa Marehemu Magomeni Mwembe chai leo.


Rais Kikwete ana Mama Salma Kikwete wakimfariji mjane wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein walikoenda kuhani msiba wa mnajimu huyo mashuhuri Magomeni Mwembe Chai leo.


Rais Kikwete akihani msiba wa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM Marehemu Athumani Mwinyimvua mtaa Matombo Magomeni Mwembe Chai leo.


Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimfariji Mama Mwajuma Mwinjum mjane wa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM marehemu Athumani Hassan Mwinjuma.



Rais Kikwete akisalimiana na watoto baada ya kuhani msiba wa Mwenyekiti wa Baraza la wazee wa CCM Marehemu Athumani Hassan Minyimvua mtaa wa Matombo Magomeni Mwembe Chai leo.

Saturday, May 21, 2011

MTANZANIA LOTUS ATIMULIWA BIG BROTHER AMPLIFIED !!!


Mwawakilishi wa Tanzania katika shindano la Big Brother nchini Afrika Kusini, Lotus Kyamba ameondolewa ndani ya jumba hilo kwa utovu wa nidhamu baada ya kugombana na mshiriki mwenzake Luclay wa Afrika Kusini.

Tukio hilo limetokea leo mchana, wakati washiriki hao walipokuwa kwenye bustani ya jumba hilo wakiendelea na zoezi maalum walilopewa na Biggie, ambako ghafla wawili hao walianza kutupiana maneno makali yakiwamo matusi, kabla ya Lotus kupandwa na munkari na kumvamia Luclay raia wa Afrika Kusini na kumzaba kibao.

Baada ya hali hiyo, uongozi wa shindano hilo uliamua kumfukuza Lotus kwa kitendo chake hicho kilichoenda kinyume na sheria za shindano.

Awali, kabla ya Lotus hajachukua uamuzi wa kumchapa kibao hicho, Luclay alianza kamtolea maneno makali ikiwemo kumkebehi kwa kumtishia Mtanzania huyo kuwa amwache, kwani yupo katika nchi yake na hawezi kumfanya kitu, jambo lililomuongezea hasira zaidi kufikia hatua hiyo ya kumvaa.

Mzozo huo uliamuliwa na washiriki wenzao, wakiwemo Mganda, Ernest, Mkenya Nic na Methiopia Danny, ambapo walimuwahi Luclay na kumsihi kutojibu mapigo na badala yake awatii.

Kitendo cha Lotus kuondoka jumbani, washiriki wenzake walimuaga kwa mara ya mwisho huku wote walionekana kuwa na huzuni kubwa, ambako Danny, Bhoke, Nic, Nkuli, Karen pamoja na Luclay walionekana kububujikwa na machozi, kwani hawakutegemea kama ingetolewa adhabu hiyo.

Kwa upande wake, Ofisa Habari Mkuu wa Multchoice Tanzania, Barbara Kambogi alisema kuwa, wamesikitishwa na jambo hilo, kwani hawakutegemea hivyo na wanajipanga kuona hali itakavyokuwa, ikiwemo harakati za kumpokea atakapotua nchini.

Shindano hilo la mwaka huu limejaa kila aina ya visa, ikiwemo ubabe kwa washiriki hao ambako karibu washiriki wote wamegombana.

SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH DR JAKAYA MRISHO KIKWETE KUFUATAIA KIFO CHA SHEIKH YAHYA HUSSEIN !!!


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Sheikh Yahya Hussein kufuatia kifo cha Mnajimu Mkuu huyo kilichotokea asubuhi ya leo tarehe 20 Mei, 2011, katika Hospitali ya Mount Ukombozi iliyoko Morocco Jijini Dar es Salaam.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Sheikh Yahya Hussein ambaye enzi za uhai wake alijipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi kutokana na kipaji chake katika masuala ya unajimu wa nyota ambao ulimpatia sifa kubwa,” amesema Rais Kikwete katika rambirambi zake.

Ameongeza: “Naomba, kama familia, mpokee salamu zangu za pole kwa kuondokewa na kiongozi muhimu na tegemeo kubwa la familia. Namuomba Mwenyezi Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya Marehemu. Amina.”

Amesema Rais Kikwete katika salamu zake: “Naelewa fika machungu mliyonayo katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wenu. Najua alikuwa mzazi, alikuwa baba, alikuwa babu, alikuwa mlezi na tegemeo kubwa la familia. Najua ameacha pengo kubwa ambalo litakuwa gumu kuzibika. Najua mko katika kipindi kigumu na cha majaribio. Hivyo nawaombeni muwe na moyo wa uvumilivu na subira. Yote ni mapenzi ya Mola. Napenda kuwahakikishieni kuwa niko nanyi katika kipindi hiki cha maombolezo ya msiba wa mpendwa wenu.”

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

20 Mei, 2011

Saturday, May 14, 2011

MARY JOEL ANYAKUA TAJI LA MISS VODACOM MISS ARUSHA CITY CENTRE 2011.!!


Mnyange Mary Joel (katikati)ndiye aliyeibuka kinara kwa kulinyakua taji la kuwa Vodacom Miss Arusha City Centre 2011 katika ngazi ya kitongoji kanda ya Kaskazini.Pembeni yake kulia ni mshindi wa pili Neema Edward pamoja na Stacey Alfred.Shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Tripple A, Arusha.

Saturday, May 7, 2011

MWANAIDI HASSANI AIBUKA MWANAMICHEZO BORA WA JUMLA TUZO ZA TASWA,RAISI MSTAAFU MH MKAPA APEWA TUZO YA HESHIMA!!


Mgeni rasmi,Makamu wa rais, Dk Gharib Bilal akimkabidhi tuzo kwa mwanamichezo wa jumala Bi Mwanaidi Hassani anayecheza mchezo wa Netball katika timu ya JKT Mbweni.Mwanaidi ndie aliyejinyakulia gari aina ya Toyota GX 100,iliyotolewa na kampuni ya Bia ya Serengeti ambao ndio waliokuwa wadhamimi wakuu wa tuzo hizo za kumsaka mwanamichezo bora wa mwaka zilizoratibiwa na TASWA,kushoto ni waziri wa Vijana,Habari,utamaduni na michezo Mh Emanuel Nchimbi akishuhudia tukio hilo.


Raisi mstaafu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Benjamini William Mkapa akipokea tuzo yake ya Heshima kutoka kwa Makamu wa Raisi Dk,Gharib Bilali.
Chama cha waandishi wa habari za michezo (TASWA)kimempa Mzee Mkapa tuzo hiyo maalumu ya Heshima kutokana na mchango wake katika michezo hasa ujenzi wa uwanja mpya wa Taifa. Mzee Mkapa amesisitiza uwanja huo uendelee kutunzwa vyema ili nchi yetu iweze kuwa na kumbukumbu na urithi kwa vizazi vijavyo.
Pichani kulia ni mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya Serengeti (SBL)Teddy Mapunda.Katika utoaji wa tuzo hizo mchezaji wa jumla ni Mwanaidi Hassani anayechezea timu ya Netball ya JKT MBWENI.

Saturday, April 30, 2011

TAMASHA LA TIGO PESA KATIKA VIWANJA VYA TANGAMANO JIJINI TANGA LEO !!!


Wasanii chipukizi toka Tanga wakitumbuiza Jukwaani.Pia katika tamasha hili wasanii mbalimbali toka Dar walikonga nyoyo za wanachi wakiwemo TMK WANAUME wakiongozwa na Juma Nature,AFANDE SELE,ROMA, 20 PERCENT.

Wakazi mbalimbali wa jiji la Tanga walijitokeza kushuhudia Tamasha hilo la Tigo Pesa lililofanyika katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga.

Watu mbalimbali wakishuhudia Tamasha hilo.

MAANDALIZI YA SAFARI YETU YA VIJANA KWENDA NCHINI HUNGARY KWA MIEZI 2 !!!


Vijana 10 wanachama wa kituo cha vijana Nguvumali Tanga.tukiwa katika ofisi zetu za kituo kujaza fomu za maombi ya Hati za Kusafiria kwa ajili ya kujiandaa na safari yetu itakayochukua miezi 2 nchini HUNGARY kutoka mwezi June 2011.Safari hii ina malengo ya kubadilishana uzoefu kati ya vijana wa nchini HUNGARY katika mji wa PECS na vijana wa TANZANIA katika jiji la Tanga.


Tukiwa nje ya ofisi ya Uhamiaji mkoa wa Tanga kufanya uhakiki wa mwisho wa fomu hizo kabla ya kuzikabidhi katika Ofisi hizo za Uhamiaji.tunashukuru sana maafisa uhamiaji mkoa wa Tanga kwa kutusaidia kwa moyo wa upendo.sasa tunasubiri maganda tu ili hatua nyingine ifuate haraka.

Wednesday, April 27, 2011

RAMSEY ATUA JIJINI DAR KUREKODI FILAMU NA WASANII WA BONGO !!!


Ramsey(kushoto)akiwa na nguli wa Filamu nchini Steven Kanumba wakizungumza na waandishi wa habari juu ya filamu hiyo.
Msanii maarufu wa Filamu toka Nigeria Ramsey Tokumbo Nouah ametinga nchini kurekodi filamu na wasanii mbalimbali wa Tanzania akiwemo Steven Kanumba.akizungumza na waandishi wa habari jana mchana katika Hotel ya Peacok jijini Dar,Ramsey amesema Filamu hiyo itakuwa ya aina yake.

Friday, April 22, 2011

OPERESHENI VUA GAMBA YA CCM YAHAMIA IRINGA !!!


Nape Nnauye na John Chiligati wakiwa na baadhi ya wanachama wa CCM

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, John Chiligati (katikati) akiwa na viongozi na wanachama wa CCM Mkoa wa Iringa, baada ya kumaliza mkutano wa hadhara kwa ajili ya oparesheni ya 'Vua Gamba' uliofanyika mjini Iringa jana. Wa pili kushoto ni Kamanda wa Vijana wa CCM, Mkoa wa Iringa, Salim

BALOZI WA UINGEREZA NCHINI AMTEMBELEA DK SHEIN IKULU ZANZIBAR !!!


Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,akimsindikiza Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,Dianne Corner, Ikulu Mjini Zanzibar jana,baada ya mazungumzo yao.


Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,akimsindikiza Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,Dianne Corner, Ikulu Mjini Zanzibar jana,baada ya mazungumzo yao.