SIKILIZA NYIMBO ZA EASYMEN HAPA:


Electronic Press Kit
Quantcast

Tazama Small Interview ya Easymen Studio Hapa:

Tuesday, July 27, 2010

ULAZWE MAHALA PEMA PEPONI DADA YETU HILDA MTENZI !!!


Aliyekuwa mtangazaji wa TBC1 mkoani Tanga Hilda Mtenzi amezikwa rasmi nyumbani kwao Manyoni.Marehemu Hilda alikuwa ni mtu mwenye kupenda ushirikiano na wadau wenzake. Ama hakika dada yetu ameacha pengo kubwa katika shirika la Utangazaji na tasnia ya habari katika Mkoa wa Tanga na Taifa kwa Ujumla. Pia marehemu Hilda ameacha mtoto mmoja.

Blog hii ya Easymen Blogspot inatoa pole kwa ndugu na marafiki wote wa marehemu.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amen.

Wednesday, July 21, 2010

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) CHAMTEUA DR,WILBROD SLAA KUWA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHADEMA !!!


Kutoka kushoto ni mwenyekiti wa chama hicho Nd Freeman Mbowe,Katikati ni Mh Dr Wilbrod Slaa na kulia ni Mh Zitto Kabwe.hapa ni katika moja ya vikao vyao vya chama.


BAADA ya kutafakari na kujaribu kushawishi watu mbalimbali, hatimaye Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kilikutana kutafuta wa kukibebea bendera katika kinyang’anyiro cha urais.

Hata hivyo, jina la Katibu Mkuu wake Dk. Wilbroad Slaa, ndilo pekee ambalo hadi jana lilikuwa linatajwa kuombwa rasmi na Chama hicho ili abebe bendera hiyo.

Kamati Kuu ya Chadema ilikuwa na kikao ambacho pamoja na ajenda zingine, moja ya ajenda hizo, ilikuwa ni kuteua jina la mgombea urais ambaye atachuana na wagombea wa CUF, CCM na TLP.

“Ninachoweza kukwambia ni kwamba Kamati Kuu imemwomba Dk. Slaa awe mgombea urais wa Chadema na amekubali,” alisema mpasha habari wetu ambaye anahudhuria vikao vya chama hicho vinavyofanyika katika hoteli moja ya Dar es Salaam.

MATUKIO YA PICHA SIKU YA KUMUAGA MFANYAKAZI MWENZETU KAZINI !!




Sunday, July 18, 2010

WEEKEND NJEMA MDAU.BURUDIKA NA NGOMA HII TOKA KWA CHIWA MAN!!



Ngoma inakwenda kwa jina la Unapocheza na mimi Audio imefanyika katika studio za Blog hii inayojulikana kama 2MOROW RECODZ.

STEVE NYERERE ASIMIKWA KUWA KAMANDA WA VIJANA BWAWANI (K) MWANANYAMALA !!!



Kamanda mpya wa Vijana CCM Tawi la Bwawani kata ya Mwananyamala Steven Mengele Nyerere, akiongea na wana CCM. mara baada ya kutawazwa rasmi kuwa kamanda wa vijana wa kata hiyo leo kwenye mkutano uliofanyika katika ofisi za tawi hilo na kuhudhuriwa na wanachama wa chama hicho, pamoja na marafiki wa msanii huo anayeigiza sauti za viongozi. "Steve Nyerere" amewashukuru marafiki zake, wazee wake mtaani, mama zake pamoja na mama yake aliyemtaja kwa jina moja la Ritah.

Friday, July 16, 2010

UKWELI KUHUSU WIMBO WA KIDUMU NITAFANYA Ft LADY JAYDEE TOKA KWA PRODUCER HERMY B !!!


Ngoja nitoe ukweli wa huu wimbo. Kidum alipokuja Dar aliamua kumtafuta Hermy B ambae alikutana nae Project FAME kule Nairobi.

Wakakutana na kufanya kazi pamoja..katika maana ya kwamba mziki huu uliundwa na Hermy na Kidumu akitoa melodies. Drum Patern Yote ni Ya hermy. Kidum aliporudi kule Nairobi akakutana na Rkay(jamaa anaetengeneza mziki wa Wahu examples Sweetlove, Runin Low) madhumuni ni kutengeneza video ya wimbo huu.

Cha ajabu Rkay akamtengeneza Kidum mpaka akakubali kurekodi upyaa wimbo huo. Rkay alikopi kila kitu ila akabadili sauti tofauti kidooogo, ila kisheria alibeba Idea ya kisanii ya Hermy kama ilivo. yote haya yalifanyika bila kuomba ruhusa wala kumpa taarifa Hermy.

Muda ulipofika Hermy alitoa huo mziki kwa radio stesheni, na kidumu alikimbilia kuomba wasiucheze huo wasubiri ule wa Rkay..alipoulizwa huu una tatizo lipi alishindwa kujieleza na akagundulika hana mantiki zaidi ya Ubaguzi wa sanaa tu. Stesheni flani flani wakakubali kuupokea na kuucheza huu wa kwetu Tanzania. Hermy hakutaka kuongea chochote kile mpaka alipoona wimbo huo wa Rkay ukichezwa na upo kwa video aliyopiga Rkay kwa sasa.

Mwenye maskio na aliyeskia wimbo huu mara ya kwanza atajua tu huu uliopo kwenye video ni tofauti na vyombo vimepunguzwa, sio kwamba Rkay hajui kutengeneza muziki, ila alikua akijaribu kujitofautisha sana na Hermy na amejikuta akiharibu kiasi flani sanaa hiyo.

Ninachoomba ni kwamba watanzania tuendelee kushikamana na kupeana suport kwenye wizi wa sanaa kama huu. Tuwe na cha kujivunia kwa watengeneza mziki wetu.
Asalaamu!

Wednesday, July 7, 2010

JANUARI MAKAMBA AJITOSA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA BUMBULI MKOANI TANGA !!


Pichani Januari Makamba


Januari Makama akiongea na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam


Nimewaiteni kwa mambo mawili. Kwanza, kuzindua kitabu nilichokiandika. Pili, kuzungumzia uvumi na minong’ono kuhusu Jimbo la Bumbuli. natarajia kugombea nafasi ya Ubunge.



Baada ya kutafakari kwa kina, na kuzungumza na wana-Bumbuli wenzangu, nimeamua niombe fursa ya kuwa sauti yao, kuwawakilisha na kuwasemea Bungeni, kuwatumikia na kushirikiana nao kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Jimbonikwetu.

Friday, July 2, 2010

KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA USHIRIKA NI KESHO TAR 3 JULY KATIKA VIWANJA VYA TANGAMANO!!




WENYEVITI WA MTAA 141 KATI YA 146 WA JIJI LA TANGA WASUSIA MAANDAMANO YA KUADHIMISHA SIKU YA SERIKALI ZA MITAA!!

Kila ifikapo tarehe 1 July ni siku ya maadhimisho ya Serikali za mitaa Nchini.Katika Jiji la Tanga hali ilikuwa tofauti ambapo Wenyeviti wa mitaa 141 kati ya 146 wa jiji hili walisusia kufanya maandamano ya Kuadhimisha siku hiyo katika jiji hili la Tanga,ambapo sherehe hizo zilifanyika katika Viwanja vya Uhuru Park na kuhudhuriwa na wenyeviti 5 tu kati ya 146 wa jiji hili.
Wenyeviti hao 141 walifanya mgomo huo kutokana na kuwa na kero mbalimbali zinazowakabili zikiwemo Halmashauri ya Jiji la Tanga kuto wajali na kuwadharau katika kuwatatulia matatizo yao ambayo ni kutoshirikishwa katika shughuli mbalimbali za maendeleo,Kutopata vitambulisho rasmi vya kutambulika kama wenyeviti wa Mitaa,Kukosa mihuri rasmi,Karatasi,Bendera za utambulisho,Ofisi za kuwahudumia wananchi ambapo kwa sasa inabidi wananchi wawafuate majumbani kwao.Posho ndogo nk.
Aidha katika maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na Madiwani,watendaji wa kata pamoja na watumishi mbalimbali wa Serikali na wananchi kwa ujumla yalileta hamasa kubwa baada ya Mgeni rasmi ambaye ni Naibu Meya wa jiji la Tanga kuuliza mbona watendaji ni kidogo alijibiwa Wamegoma.na naibu meya huyo kuahidi kushughulikia suala hilo baadae.

TIMU YA VIJANA YA MKOA WA TANGA ILIYOKUWA IKISHIRIKI KWENYE COPA COCA COLA YAFUNGIWA KUENDELEA NA MASHINDANO HAYO.!!

Timu ya Vijana wadogo ya mpira wa miguu ya Mkoa wa Tanga iliyokuwa ikishiriki kwenye Fainali za Copa CocaCola zilizokuwa zinaendelea jijini Dar es Salaam imefungiwa kuendelea na Mashindano hayo huku Viongozi wa Timu hiyo kufungiwa Kushiriki katika Shughuli za Kisoka kwa muda kati ya miezi 6 hadi miaka 2.
Hatua hiyo imechukuliwa na Shirikisho la Michezo wa Kandanda Tanzania TFF jana jioni baada ya Kubaini kuwa na udanganyifu wa Umri pamoja na kughushi majina kwa wachezaji 2 wa timu hiyo ya Tanga.
Awali Timu hiyo ya Mkoa wa Tanga ilikuwa inashikilia nafasi ya Pili ambayo ilitakiwa kucheza nusu fainali na badala yake nafasi hiyo inachukuliwa na timu ya mkoa wa Mbeya.
Kwa upande wa wadu wa michezo wa Mkoa wa Tanga wamesikitishwa kwa hatua hiyo iliyochukuliwa lakini pia kwa upande mwengine Viongozi wa mchezo huo kwa mkoa wa Tanga watajifunza kutokana na vitendo vyao viovu mbele ya Tasnia ya Michezo na Mkoa kwa Ujumla.

KWA HERI MARCIO MAXIMO TUTAKUKUMBUKA KWA MENGI KIMICHEZO !!


Aliyekuwa kocha Mkuu wa Taifa Stars, Marcio Maximo, ameagwa rasmi na wadau mbalimbali wa michezo katika hafla fupi iliyoandaliwa na TFF Msasani jirani na shule ya Feza jijini Dar es salaam. Katika hafla hiyo, pamoja na mambo mengine, Kocha Maximo alipewa zawadi mbalimbali ikiwemo ya kinyago alichopewa na Mwenyekiti Mtendaji wa kiwanda cha Serengeti, Jaji Mark Bomani.
Ni dhahiri kwamba kocha huyo atakumbukwa kwa kazi yake aliyoifanyia Tanzania japokuwa bado kuna wadau wa soka ambao wanasema hakufaya kitu ila tunaojua kusema asante tunasema Maximo amefanya kitu kikubwa katika soka letu lililokuwa la kichwa cha Mwendawazimu enzi hizo, na anastahili kupongezwa mpaka hapa alipotufikisha manake kuna methali inayosema "Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake mpeni"
Yote kwa Yote tunasema Watanzania tunajifanya tunajua sana mpira wakati kujua kwetu kuko vinywani zaidi kuliko vitendo na kama ndiyo hivyo basi tukubali kwamba hatujui jamani.



Kocha Maximo akiwa na baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa wakati wa sherehe ya kumuaga.