SIKILIZA NYIMBO ZA EASYMEN HAPA:


Electronic Press Kit
Quantcast

Tazama Small Interview ya Easymen Studio Hapa:

Thursday, March 31, 2011

NAIBU WA MAWASILIANO SAYANSI NA TEKNOLOJIA ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA ZANTEL !!!


Ofisa Mkuu wa Tekenolojia Kampuni ya Zantel Bw. Moncef Mettiji wa pili (pili kulia) akimuonesha moja ya mitambo ya mawasiliano ya Kampuni hiyo, Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Bw. Charles Kitwanga alipotembelea kampuni hiyo Dar es salaam leo kuliani, Ofisa Mtendaji Mkuu Ali Bin Jarsh na kushoto ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa wa Zantel, Norman Moyo.

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO SAYANSI NA TEKNOLOJIA ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA ZANTEL !!!


Ofisa Mkuu wa Tekenolojia Kampuni ya Zantel Bw. Moncef Mettiji wa pili (pili kulia) akimuonesha moja ya mitambo ya mawasiliano ya Kampuni hiyo, Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Bw. Charles Kitwanga alipotembelea kampuni hiyo Dar es salaam leo kuliani, Ofisa Mtendaji Mkuu Ali Bin Jarsh na kushoto ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa wa Zantel, Norman Moyo.

BURUDIKA NA VIDEO HII YA MSANII SAJNA FT LINAH !!!

Tuesday, March 22, 2011

POLENI SANA FAMILIA NA BENDI YA MUZIKI YA 5 STAR MODEN TAARAB KWA MSIBA MKUBWA WA KUONDOKEWA NA WASANII 13 KATIKA AJALI YA GARI HAPO JANA USIKU.!!!


Baadhi ya wasamaria wema waliokuwa kenye foleni ya magari baada ya kutokea kwa ajali ya basi dogo la wasanii wa kundi la 5 STAR Moden Taarab wakichunguza kwa makini iwapo kuna mtu aliyebanwa ama kusahauliwa kuokolewa ama mwili wake kubakia eneo hilo baada ya basi hilo kuparamia lori lililosheheni Mbao lililokuwa limeharibika njiani.katika barabara kuu ya Iringa - Morogoro,eneo la hifadhi ya Taifa ya Wanyama ya Mikumi,karibu na kijiji cha Doma,Wilaya ya Mvomero usiku wa kuamkia leo.

Lori lililoparamiana na basi la wanamuziki wa bendi ya 5 Stars Moden Taarab.

Msanii wa kikundi cha Taarab cha East African Melody,Bi Mwanahawa Ally.akiwa wodini katika Hospitali ya wilaya ya Morogoro leo baada ya kujeruhiwa katika ajali ya basi dogo la wasanii wa Kundi la Five Stars Moden Taarab la jijini Dar es Salaam.
Yeye alikuwa msanii mualikwa katika safari hiyo ya kikazi katika mikoa ya nyanda za juu Kusini.

Blog hii ya EAZYMEN.inatoa pole kwa familia zote zilizopatwa na misiba ikiwa ni pamoja na majeruhi na Bendi nzima ya 5 Stars Moden Taarab.Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi Ameni.!!!

Sunday, March 13, 2011

Saturday, March 12, 2011

WIKI HII NILITEMBELEA OFISI ZA EMPTY SOULZ PRODUCTION DAR ES SALAAM !!!!


Siku ya Jumatatu iliyopita nilifanya ziara ndogo ya kuwasalimu rafiki zangu wa Emptysoulz Production jijini Dar es Salaam.hapa nikila pozi Empty Soulz.


Ukifika katika Ofisi za Empty Soulz lazima utakutana na Sign hii mlango wa kuingia ofisi zao.


Mimi Pashua na rafiki yangu H Baba tulikutana Emptysoulz na kubadilishana mawazo ya hapa na pale na pia kumpongeza kwa kuwa mfungaji wa Mabao yote mawili dhidi ya Bongo Movie.

Thursday, March 10, 2011

YALIYOJIRI KATIKA SHOW YA MSANII ROMA NDANI YA CLUB LA GRANDE LACASA CHICA IJUMAA ILIYOPITA !!!

Msanii wa kizazi kipya ROMA akiwa jukwaani akiwakilisha Hip Hop ya ukweli kwa mashabiki waliofika kumpa sapport ndani ya La Grande La Casa Chica.

Msanii ROMA akiwa jukwaani akiwakonga mioyo mashabiki kwa staili za hatari.

ROMA akiwa jukwaani akiwakilisha.kwa kweli wakazi wa Tanga walimpa Support ya kutosha Kwa kuwa Mcheza kwao Hutunzwa.

Show love mimi Pashua kushoto, Young Dee katikati na mshkaji Kibua toka Moshi.

Mimi Pashua na Belle 9.

Msanii Belle 9 akiwa jukwaani aliwakilisha ipasavyo na alipata shangwe nyingi sana kutoka kwa wakazi wa Tanga ndani ya La Grande la Casa Chica.

Belle 9 jukwaani akiwakonga nyoyo mashabiki.

Msanii Young Dee akiwa jukwaani naye aliwakilisha vilivyo kwa kutoa burudani ya Kutosha kiasi cha kupta shangwe nyingi sana.

Young Dee jukwaani akiwakilisha.

Miss T au Tayana nae alikuwapo ndani ya nyumba na hapa akiwasabahi mashabiki.

Hawa ni baadhi ya warembo wa wanaowania Umiss kitongoji cha Tanga Central walikuwepo kumpa Sapport Msanii ROMA.

Kundi maarufu la Dancers toka jijini Tanga la TOWN BOYZ wakiwakilisha jukwaani katika kumpa support ROMA.

Saturday, March 5, 2011

EMPTY SOULZ PRODUCTION KUPITIA STUDIO ZAO MPYA ZA AUDIO SEDUCTIVE RECORDS WATAMBULISHA NYIMBO MPYA YA MSANII OCHU !!!!
POLENI KWA UJENZI WA TAIFA NA NAAMINI MU WAZIMA WA AFYA TELE

STUDIO MPYA YA SEDUCTIVE RECORDS INAPENDA KUWAPA NAFASI WADAU, MARAFIKI NA WAPENZI WOTE WA MUZIKI WA BONGO FLEVA KUSIKILIZAA SINGLE YA PILI YA MSANII OCHU EDDY SHEGGY AU KWA JINA LA KISANII OCHU

SINGLE HIYO INAITWA "UMECHAKACHUWA" IMEREKODIWA NA PRODUCER JILLY BABY WA SEDUCTIVE RECORDS NA PIA IMESHAFANYIWA MUSIC VIDEO YAKE CHINI YA KAMPUNI YA EMPTYSOULZ PRODUCTION AMBAYO IMESHAANZA SAMBAZWA KATIKA VITUO MBALIMBALI VYA TV.

NATUMAINI MTAENJOY KAZI HII NZURI NA PIA KUMPA SUPPORT MSANII HUYU AMBAYE ANAJARIBU KUENDEREZA SANAA HII ALIYOKUWA AKIIFANYA MAREHEMU BABA YAKE MSANII WA MUZIKI WA DANCE EDDY SHEGGY.

PIA USISITE KUANDIKA KUTOA USHAURI PALE UTAPOSIKILIZA SINGLE HII YA "UMECHAKACHUWA"

ASANTENI NA TUWE PAMOJA!

Regards:

Solomon Lamba

WADAU KUMRADHI KWA KUTOPATA NEW UPDATE NI MATATIZO YA NET TANGA !!!

WADAU SAMAHANINI KWA KUTOWEKA UPDATE TOKA JANA HII NI KUTOKANA NA MATATIZO YA NET KATIKA MKOA WA TANGA.HAIWEZEKANI HATA KUAPLOAD PICTURE,NET IKO SLOW SANA.ILA PUNDE NET IKIRUDI HALI YAKE TUTAWEKA HABARI MPYA.