SIKILIZA NYIMBO ZA EASYMEN HAPA:


Electronic Press Kit
Quantcast

Tazama Small Interview ya Easymen Studio Hapa:

Sunday, May 22, 2011

RAISI JAKAYA MRISHO KIKWETE AHANI MISIBA YA SHEIKH YAHYA NA MZEE ATHUMANI MWINJUMA LEO !!


Rais Kikwete akipokewa na Hassan Yahya Hussein, Mtoto mkubwa wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein alipokwenda kuhani msiba wa mnajimu huyo maarufuf nyumbani kwa Marehemu Magomeni Mwembe chai leo.


Rais Kikwete ana Mama Salma Kikwete wakimfariji mjane wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein walikoenda kuhani msiba wa mnajimu huyo mashuhuri Magomeni Mwembe Chai leo.


Rais Kikwete akihani msiba wa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM Marehemu Athumani Mwinyimvua mtaa Matombo Magomeni Mwembe Chai leo.


Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimfariji Mama Mwajuma Mwinjum mjane wa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM marehemu Athumani Hassan Mwinjuma.Rais Kikwete akisalimiana na watoto baada ya kuhani msiba wa Mwenyekiti wa Baraza la wazee wa CCM Marehemu Athumani Hassan Minyimvua mtaa wa Matombo Magomeni Mwembe Chai leo.

Saturday, May 21, 2011

MTANZANIA LOTUS ATIMULIWA BIG BROTHER AMPLIFIED !!!


Mwawakilishi wa Tanzania katika shindano la Big Brother nchini Afrika Kusini, Lotus Kyamba ameondolewa ndani ya jumba hilo kwa utovu wa nidhamu baada ya kugombana na mshiriki mwenzake Luclay wa Afrika Kusini.

Tukio hilo limetokea leo mchana, wakati washiriki hao walipokuwa kwenye bustani ya jumba hilo wakiendelea na zoezi maalum walilopewa na Biggie, ambako ghafla wawili hao walianza kutupiana maneno makali yakiwamo matusi, kabla ya Lotus kupandwa na munkari na kumvamia Luclay raia wa Afrika Kusini na kumzaba kibao.

Baada ya hali hiyo, uongozi wa shindano hilo uliamua kumfukuza Lotus kwa kitendo chake hicho kilichoenda kinyume na sheria za shindano.

Awali, kabla ya Lotus hajachukua uamuzi wa kumchapa kibao hicho, Luclay alianza kamtolea maneno makali ikiwemo kumkebehi kwa kumtishia Mtanzania huyo kuwa amwache, kwani yupo katika nchi yake na hawezi kumfanya kitu, jambo lililomuongezea hasira zaidi kufikia hatua hiyo ya kumvaa.

Mzozo huo uliamuliwa na washiriki wenzao, wakiwemo Mganda, Ernest, Mkenya Nic na Methiopia Danny, ambapo walimuwahi Luclay na kumsihi kutojibu mapigo na badala yake awatii.

Kitendo cha Lotus kuondoka jumbani, washiriki wenzake walimuaga kwa mara ya mwisho huku wote walionekana kuwa na huzuni kubwa, ambako Danny, Bhoke, Nic, Nkuli, Karen pamoja na Luclay walionekana kububujikwa na machozi, kwani hawakutegemea kama ingetolewa adhabu hiyo.

Kwa upande wake, Ofisa Habari Mkuu wa Multchoice Tanzania, Barbara Kambogi alisema kuwa, wamesikitishwa na jambo hilo, kwani hawakutegemea hivyo na wanajipanga kuona hali itakavyokuwa, ikiwemo harakati za kumpokea atakapotua nchini.

Shindano hilo la mwaka huu limejaa kila aina ya visa, ikiwemo ubabe kwa washiriki hao ambako karibu washiriki wote wamegombana.

SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH DR JAKAYA MRISHO KIKWETE KUFUATAIA KIFO CHA SHEIKH YAHYA HUSSEIN !!!


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Sheikh Yahya Hussein kufuatia kifo cha Mnajimu Mkuu huyo kilichotokea asubuhi ya leo tarehe 20 Mei, 2011, katika Hospitali ya Mount Ukombozi iliyoko Morocco Jijini Dar es Salaam.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Sheikh Yahya Hussein ambaye enzi za uhai wake alijipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi kutokana na kipaji chake katika masuala ya unajimu wa nyota ambao ulimpatia sifa kubwa,” amesema Rais Kikwete katika rambirambi zake.

Ameongeza: “Naomba, kama familia, mpokee salamu zangu za pole kwa kuondokewa na kiongozi muhimu na tegemeo kubwa la familia. Namuomba Mwenyezi Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya Marehemu. Amina.”

Amesema Rais Kikwete katika salamu zake: “Naelewa fika machungu mliyonayo katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wenu. Najua alikuwa mzazi, alikuwa baba, alikuwa babu, alikuwa mlezi na tegemeo kubwa la familia. Najua ameacha pengo kubwa ambalo litakuwa gumu kuzibika. Najua mko katika kipindi kigumu na cha majaribio. Hivyo nawaombeni muwe na moyo wa uvumilivu na subira. Yote ni mapenzi ya Mola. Napenda kuwahakikishieni kuwa niko nanyi katika kipindi hiki cha maombolezo ya msiba wa mpendwa wenu.”

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

20 Mei, 2011

Saturday, May 14, 2011

MARY JOEL ANYAKUA TAJI LA MISS VODACOM MISS ARUSHA CITY CENTRE 2011.!!


Mnyange Mary Joel (katikati)ndiye aliyeibuka kinara kwa kulinyakua taji la kuwa Vodacom Miss Arusha City Centre 2011 katika ngazi ya kitongoji kanda ya Kaskazini.Pembeni yake kulia ni mshindi wa pili Neema Edward pamoja na Stacey Alfred.Shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Tripple A, Arusha.

Saturday, May 7, 2011

MWANAIDI HASSANI AIBUKA MWANAMICHEZO BORA WA JUMLA TUZO ZA TASWA,RAISI MSTAAFU MH MKAPA APEWA TUZO YA HESHIMA!!


Mgeni rasmi,Makamu wa rais, Dk Gharib Bilal akimkabidhi tuzo kwa mwanamichezo wa jumala Bi Mwanaidi Hassani anayecheza mchezo wa Netball katika timu ya JKT Mbweni.Mwanaidi ndie aliyejinyakulia gari aina ya Toyota GX 100,iliyotolewa na kampuni ya Bia ya Serengeti ambao ndio waliokuwa wadhamimi wakuu wa tuzo hizo za kumsaka mwanamichezo bora wa mwaka zilizoratibiwa na TASWA,kushoto ni waziri wa Vijana,Habari,utamaduni na michezo Mh Emanuel Nchimbi akishuhudia tukio hilo.


Raisi mstaafu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Benjamini William Mkapa akipokea tuzo yake ya Heshima kutoka kwa Makamu wa Raisi Dk,Gharib Bilali.
Chama cha waandishi wa habari za michezo (TASWA)kimempa Mzee Mkapa tuzo hiyo maalumu ya Heshima kutokana na mchango wake katika michezo hasa ujenzi wa uwanja mpya wa Taifa. Mzee Mkapa amesisitiza uwanja huo uendelee kutunzwa vyema ili nchi yetu iweze kuwa na kumbukumbu na urithi kwa vizazi vijavyo.
Pichani kulia ni mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya Serengeti (SBL)Teddy Mapunda.Katika utoaji wa tuzo hizo mchezaji wa jumla ni Mwanaidi Hassani anayechezea timu ya Netball ya JKT MBWENI.