Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa leo na Rwanda ambapo hadi Dakika 90 zilitoka sare ya bao 1-1.katika kipindi cha kwanza Taifa Stars ilionyesha kuzidiwa hali iliyosababisha kufungwa goli katika dakika za mwanzo wa mchezo.
Lakini katika kipindi cha pili baada ya Taifa Stars kufanya mabadliko ya kumtoa Geofrey Bony na Kumuingiza Mussa Hassan Mgosi waliweza kuonyesha mchezo mzuri ulipoelekea kukomboa goli walilofungwa na kupelekea hadi dakika 90 kutoka sare ya 1-1.
Matokeo haya yanaipa Taifa Stars wakati mgumu sana katika mchezo wa marudiano utakaofayika Rwanda.hivyo inatakiwa ishinde na Droo yoyote haitaisadia Taifa stars kusonga mbele katika kufuzu kucheza fainali za michuano ya Mataifa ya Africa kwa wachezaji wa ndani(CHAN).
No comments:
Post a Comment