Raisi wa Nigeria Umaru Yar'Adua (pichani) amefariki dunia siku ya Jumatano mwezi wa tano akiwa na miaka 58. Marehemu Yar'Adua alikuwa na matatizo ya moyo pamoja na figo.
Marehemu Yar'Adua atazikwa leo siku ya Alhamisi mchana katika kijiji cha Katsina nchini Nigeria.Yar'Adua hakujishughulisha na mambo ya siasa tangu mwezi wa kumi na moja alipokuwa ameenda kutibiwa nchini Saudia Arabia.
Alirudi chini Nigeria mwezi wa pili lakini alishindwa kuendesha shughuli za kiserikali kutokana na kuumwa.Msaidizi wa Raisi Mh. Goodluck Jonathan atashikilia madaraka mpaka mwezi wa utakapofanyika uchaguzi mwingine mwezi wa nne 2011.
Marehemu Yar'Adua alikuwa ni msomi wa kwanza kutoka cho kikuu kuchukua madaraka, alishinda uchaguzi mwezi wa nne mwaka 2007.Yar'Adua alipewa jina la "Baba Go-Slow", kutokana na utendaji wake wa kazi.
Historia yake.Yar'Adua, alizaliwa katika mji wa Katsina mwezi wa nane tarehe 16 mwaka 1951, alikuwa muislamu.Ametokea katika familia yenye kufuata mchakato wa kisiasa. Baba yake alikuwa waziri na kaka yake alikuwa mtu wa pili katika serikali ya Raisi Obasanjo's toka mwaka 1976 mpaka 1979.Alisoma katika chuo kikuu cha Ahmadu Bello University Zaria kutoka mwaka 1972 mpaka 1975 masomo ya Chemist.
Amesomea masomo ya MSc toka 1978-1980.Alianza kusomesha Chemistry kabla ya kuingia katika biashara mwaka 1980s alikuwa mkurugenzi katika kampuni ya Sambo Farms Ltd katika mji wa Katsina.Alichaguliwa kuungoza mji wa Katsina 1999 na kuchaguliwa tena kuongoza mji huo mwaka 2003.
Maremu Yar'Adua alioa mwaka 1975 alijaaliwa kupata watoto saba.
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi.Amina
Thursday, May 6, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment