SIKILIZA NYIMBO ZA EASYMEN HAPA:


Electronic Press Kit
Quantcast

Tazama Small Interview ya Easymen Studio Hapa:

Wednesday, May 26, 2010

IJUE TAASISI YA KUKUZA NA KUUTANGAZA UTALII MKOA WA TANGA INAJULIKANA KAMA TANGA TOURISM NETWORK ASSOCIATION (TATONA) !!!

Blog yenu ya Easymen leo ilipata bahati ya kutembelea ofisi za Taasisi ya Kutangaza na Kukuza Utaalii katika Mkoa wa Tanga ijulikanayo kama Tanga Tourism Network Association (TATONA).Ofisi za Taasisi hii zipo katika Jengo la Sachak House mkabala na Posta kuu ya Tanga au karibu kabisa na Mahakama ya Mwanzo.



Mimi nikishow love na Laurent (mwenye shati la blue) ambaye ni katibu wa Taasisi hiyo ya TATONA.


Ofisi ya TATONA


Laurent Akiwa Ofisini akila mzigo.




Kwa mujibu wa Laurent ameiambia blog hii kuwa Taasisi hiyo ipo katika hatua za mwisho kabis za kuanzisha Website yake ili kurahisisha upatikanaji wa Taarifa za Utalii.
Pia allidokeza blog hii kwamba wako katika Maandalizi ya Kwenda Arusha katika Maonyesho ya Utalii yajulikanayo kama KARIBU FAIR yatakayoanza tarehe 2 hadi 6 June 2010.





Monday, May 24, 2010

MJUE MSANII TOKA TANGA AMBAYE KWA SASA ANISHI UK.TIZZLE!!!

Msanii kutokea jijini Tanga anayejulikana kwa jina la Tizzle ambaye hivi sasa anaishi nchini Uingereza kuonako jiji la London, amechia ngoma yake mpya inayoitwa 'Nameless' aliyomshirikisha Damuz.

Akiongea na Blog hii moja kwa moja kutokea Uingereza leo amesema kuwa ngoma hiyo ameifanya pale studio za East London kwenye studio moja inaitwa Mzuka Entertainment Rec chini ya producer Josh.

Tizzle aliongeza kuwa, anaamini ngoma hiyo itamuweka pazuri kunako ramani ya Bongo Flava na duniani kwa ujumla kwa kuwa ina kiwango cha kimataifa.




Tizzle ambaye kabla ya kwenda Uingereza alikuwa anaishi pale Majani Mapana na baadae kuhamia Bara Bara ya 15, kwa sasa yupo anajipanga kutoka na ngoma nyingine ya 'Hisia Zangu' ambayo atawashirikisha washkaji zake damuz, josh pamoja na danny.
Pia alisema mpango wa albamu unakuja na ataipa jina punde tu itakapokamilika. Stay tune to this Blog.



HATIMAYE MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU YATOA HUKUMU YA MIAKA 2 JELA KWA AMATUS LIYUMBA!!!


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo imesoma Hukumu dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Amatus Liyumba,Katika hukumu hiyo Liyumba amepatikana na hatia na kuhukumiwa kwenda jela miaka miwili dhidi ya kesi ya utumiaji mmbaya wa madaraka .
Hata hivyo jopo la wanasheria na mawakili wake wamesema hawakuafiki hukumu hiyo na hivyo wanatarajia kukata Rufaa.

SIMBA UWANJANI TENA LEO KUVAANA NA APR YA RWANDA, KILA LA KHERI !!!!

Timu ya Soka ya Simba Sports Club leo inatarajiwa kushuka Dimbani kuvaana na APR ya Rwanda katika mchezo wa Robo Fainali za Kombe la Kagame Cup zinazoendelea nchini Rwanda.

Sunday, May 23, 2010

TWIGA STARS YAIBANJUA ERITREA MABAO 8 -1 !!!

Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu wanawake maarufu kama Twiga Stars Jana iliweza kuwadhihirishia watanzania kwamba wako fiti baada ya kuilaza mabao 8 - 1 timu ya wanawake ya Eritrea,mchezo uliofanyika katika uwanja wa Uhuru.
Hongereni sana Twiga Stars kwa kututoa Kimasomaso watanzania.

HUKUMA YA KESI YA LIYUMBA KUTOLEWA LEO MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU !!!

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Leo inatarajiwa kusoma Hukumu dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Amatus Liyumba.

BAADA YA MVUA KUBWA KUNYESHA BAADHI YA MAKAZI KATIKA MAENEO YA DUGA JIJINI TANGA YAPO KATIKATI YA MAJI !!!!





Baadhi ya Wakazi wa Maeneo ya Duga Shamsil Maarif jijini Tanga wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na Maji mengi yaliyozunguka nyumba zao yaliyotokana na Mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha na hadi kupelekea kuingia ndani ya Nyumba zao na kusababisha uharibifu wa Thamani (Fenicha).
Picha juu na chini ni taswira halisi ya makazi hayo katika majira ya leo mchana.baada ya Blog yenu ya Easymen ilipotembelea maeneo hayo na kujionea hali halisi.
















Saturday, May 22, 2010

HATIMAYE MRISHO NGASA KATUA AZAM FC RASMI !!!

Mchezaji wa Zamani wa Club ya Young African Mrisho Ngasa amefanikiwa kujiunga na Timu ya Azam Fc.kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Yanga Iman Madega siku ya jana alitamka rasmi kwamba Mrisho Ngasa sasa ni mchezaji halali wa timu ya Azam Fc.Mrisho ngasa amenunuliwa na Azam Fc kwa ada ya Uhamisho ya kitita cha Tsh Milioni hamsini na nane ( 58,000,000).

LUSHOTO KUMPATA MNYANGE WAKE TAREHE 29 MWEZI HUU!!


Wednesday, May 19, 2010

CHANGIA CCM KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2010 !!











Juma Nature
Chege


Dully Sykes

Belle 9 na Diamond Platinum



TUSIKIE UJUMBE HUU TOKA KWA ROMA (Mr President) KUHUSU TUZO ZA KILI!!

Reports:- “Habari yako bana….hop unaendelea poa na kazi, ni hivi ndugu yangu, niliwahi kuambiwa msemo fulani, kuwa katika kila utakalofanya au litakalotokea basi lazima watu wataongea, kwamba ulichofanya sio sahihi. Ikiwa ina maana kuwa watu mara zote hawaridhiki na kile kinachotokeaga.
Nikapewa na mfano pia, kwamba kulikuwa na baba na mtoto na punda wanaenda sehemu ya mbali. Basi yule baba alimpakiza mwanae juu ya punda, huku yeye baba mtu akitembea kwa miguu, watu kuona vile wakasema eti oooh!! baba anamdekeza mwanae, iweje ampakize juu ya punda, basi baba akaamua amshushe mwanae then baba akapanda yeye punda huku mtoto anatembea, pia watu wakasema baba anamtesa mwanae,
baba akaona sio kesi wakapanda wote yule punda, watu pia wakasema tena, kuwa hakuna haki za wanyama?Iweje wamtese yule punda? Iweje punda m1 apandwe na watu wawili? Basi baba alichoamua ni yeye na mwanae kushuka na kutembea kwa miguu huku punda akitembea mwenyewe, alidhani ndo’ afadhali lakini aaaah waaapi!! watu wakasema tena, etii ooh yule mzee hana akili, hajui kutumia vitendea kazi, yaani punda yupo halafu anatembea kwa miguu….ha ha ha ha ha!!!
Kwanini nimetoa mfano huu? kwa sababu hiyo niliyosema hapo juu kwamba watu lazima wataongea tu!! kwa kila kitakachotokea,LAKINI SIO MARA ZOTE WANAONGEA KIMAKOSA TUU, wakati mwingine matatizo yanaonekana wazi, kwahiyo lazima yaongelewe….BACK IN BUSINESS….. TUZO/TUNZO za kili, naamini TUZO ndio sahihi …nway, zimetolewa juzi kati na waliopata wamepata…aya nawapa hongera zao, maana wametengeneza historia ya maisha ya mziki wao, lakini je kweli wanastahili kupata tuzo hizo? wanastahili kuwepo kama nominees katika hizo categories?
Wanafanya aina hiyo ya mziki ambao wameshindia hiyo tuzo? haya ni maswali ya kujiuliza, siwafahamu waliopo kwenye kamati husika ya tuzo hizi, ila naamini watakuwa na uelewa wa mziki wetu, lakini kwa hili la kutokea kila mwaka linanipa mashaka.Hivi tunawezaje kusema basketball imepiga hatua ikiwa kila ligi, kila mwaka timu zinazoingia fainali ni SAVIO na VIJANA? kikapu kitakuwa hakijakua maana vipawa vipya havionekani? au nyie mnatazama katika nyanja zipi? kama sio hizi za baada ya kazi ngumu lazima utunukiwe tuzo.
Jee kweli havionekani? Na kipi kinasababisha visionekane? na je hilo sio jukumu la hawa waandaaaji wa tuzo hizo?Obviously itakuwa ni jukumu lao, maana kati ya hao waandaaji naamini wapo maproducers, nadhani hata mapresenters na d.j’s wa radio na t.v pia na wadau kwa ujumla wa mziki huu pia…..!! 2009-2010 binafsi naamini kabisa game ya mziki wetu ilibadilika sana, na kutawaliwa na chipukizi, ambao wengi wamefanya vizuri sana kuliko hawa wasanii wengine ambao wapo kwenye game kwa muda mrefu. Izzo b, nikki wa pili, roma, Quick r…., diamond, belle9, lina, barnaba, pipi, amini, na wengineo wengi,
siwezi kuwataja wote na haina maana kuwa kama sijakutaja hapa ndo’ hufai…. lah hasha!!Hayo ni baadhi ya majina yaliyonijia haraka tu, hawa mbona walifanya vizuri na waliweza kusimama bora zaidi…je tunawaingiza kwenye category moja tu ya msanii anaechipukia? hapana…mbona ktk category ya msanii bora wa RnB yupo steve, Belle 9, diamond, A.T, hawa wengi wao ni chipukizi kama sio wote…which means waliweza kufanya vizuri zaidi ya wale waliotangulia kwenye game hii, si ndio?Haya tuangalie na upande mwingine wa shilingi, je tukirudi kwa upande wa wanaofanya mziki wa RAP…
ina maana hawa hawakupata upinzani kutoka kwa upcomingz artists wengineo zaidi ya Quick r….. tu?mbona kila mwaka ni kama nominees ni walewale tu wanajirudia?mziki (rap game)tuseme haikui?wao ndo’ bora kila mwaka kweli? ha ha ha ha ha!! ni Quick r…peke yake ndo aliweza kucompete na hawa watu tu? What about roma? Na je nikki wa 2?Business nae pia? hata kala jeremiah pia?
Au ni vigezo gani vinatazamwa katika hili? Na hao nominees wote au wengi wao wame base kwenye topic moja tu, kujisifu wao ndio wanai-run hii game kuliko wengine, huyu anajiita professional , yule anasema anatuvua kama samaki, huyu nae anatuambia tumpishe, huku anatupigia honi…. pom pom pom pishaaaa. IZ DAT HIP HOP????mtu anasema NINA PESA MINGI MPAKA NATAMANI JITEKA…THEN WATU WAPO KING STONE KAMA JAMAICA….thats hip hop????? vipi kuhusu huyu aliyesema…. MIGOMO YA CHUO KIKUU NAITUPIA JICHO LA TATU…SITETEI MPAKA RUTASHOBORWA AKIWA WAKILI KISUTU…
Kwa tafsiri ya haraka haraka nani anafanya hip hop real kati ya hawa? nani anaongea real? ni kweli ana pesa nyingi kiasi hicho hadi anatamani kujiteka? Nway HIP HOP ina vitu vingi ikiwemo consciousness na free styl pia, pengine yoyote atakayechagua moja wapo kati ya hivyo vitu viwili atakuwa ameitendea haki, so may be wana diserve. Msiseme kuwa siku zote nilikuwa wapi sikuongea, maana maneno hayaozi na ukweli utaendelea kuwepo tu.Sitaki kuliongelea hili la HIP HOP, lakini nitaligusia, wengi wanaamini mziki wa HIP HOP ni ule unaozungumzia REALITY,(maisha halisi),kutetea haki, kutoa elimu, kukosoa nakadhalika, but i-base katika sense na consciousness, lakini tunaona nominees wa categories kama hizo hawahusiani na huo uhalisia wa HIP HOP, mfano halisi kwenye nyimbo zao hizo zilizoshiriki? au HIP HOP ni kuwa na beat ngumu tu? ha ha ha ha ha!! nway hata wenzetu wa America tunaona katika hili pengine wanasuasua ndomana nasi pia, kwa maana vingi tunavitoa kwao.Mashabiki ambao ndo ‘ wanapiga kura, wengi wao hawafuatilii mziki kwa undani na umakini zaidi, mimi naamini hilo, mfano nitakupa……..”
watakapoona kwenye category ya muandishi bora wa nyimbo ya RAP yupo ROMA na ngoma yake ya MR.RESIDENT na yupo na flani na wimbo wake ambao kimsingi huyo flani amesifia tu pombe na starehe za club, hata kama huo wimbo hauna maana, lakini kwa vile tu huyo msanii flani ana album, ni mkongwe, anajulikana sana na alitamba na ngoma nyingi sana basi utakuta shabiki ana vote kwa huyo msanii flani, pasipo kujua tuzo inataka nini katika hiyo category…tena utamkuta anasema aaaah!!ROMA mtoto wa juzi tu atamuweza huyu flani, huyu mkongwe sana, huyu flani alihit na ngoma yake ile ya………….apo anakumbushia ngoma ya nighteen kweusiiiii….wakati award haitaki nyimbo hiyo… hicho ndicho mashabiki wengi wanakifanya….. Hivi tujadiliane hili unaposema watu watume sms kumchagua msanii bora wa kitu flan, halafu yule artist akawapanga watu wake wampigie kura na wakampigia kura akashinda, je hapo tutakuwa tumemchagua yeye kama bora au? ok sio asilimia zote za kura hutoka kwa wananchi, je nyie majaji mnaangalia vigezo gani? nafahamu kwenye mkutano wenu kabla ya kuanza kuvote mlitaja vigezo vyenu, lakini bado nina shaka na hilo.
Ili msanii afanye vizuri anatakiwa awe na presentation nzuri, production safi na promotion pia iwe ya nguvu zaidi, lakini kwetu hapa bongo hutokea mara chache sana hivyo vitu kuwa kama vigezo vya kufanya vizuri, itz like hakuna formula inayomfanya mtu akafanya vizuri hapa kwetu, tunaona wasanii wanatoa nyimbo za ajabu ajabu lakini zinaheat, sasa nauliza huo ubora wanaoutazama killi award je ni kwa ajili ya air tym hiyo wanayopata hao wasanii au?kama ndivyo je yule atakayeweza kujifanyia air time ya nguvu kubwa ndio ataibuka mshindi? Pengine mimi sijajua ubora wa nyimbo ni upi?Labda ni midundo iwe mikali na vocal ziwe safi na sound iwe poa halafu humo katikati utupie mashairi yako ya mitindo huru yasiyokuwa na maana katika kiwango cha kutosha…… Sitaki na sipendi mtu anaposema mbona America wanafanya hivi…kwani si wao!!ok sisi tunacopy kwao lakini isiwe kila kitu jamani, tukishindwa kabisa sawa tuvicopy, lakini tutazame na sehemu ya kuvipaste pia jamani.
Wimbo bora wa mwaka, je ni bora kuanzia tungo, midundo, upangiliaji wa mashairi,sauti,style na vingine muhimu? au ni bora kwa sababu unajulikana sana na watu wanaiimba hadi watoto!!Je huo ndo ubora? na yule ambae hajajulikana wala kusikika sana je yeye siyo bora? Basi ni vema hata majina ya categories yakabadilishwa pia. Labda tuite wimbo uliopigwa sana na vituo vya radio, au club, msiniambie kama kilichobora ndo’ hupigwa, eti kama sio bora kisingepigwa…aaaah waaapi….!!mapepe ya kingwendu au kamongo ya mr.ebbo zilipigwa sana kipindi hicho,….pengine zilikuwa bora, mimi sina comments hapo.
Nafahamu wengi wakipata tuzo hakuna hata mmoja atakayeweza kusema hazipo fair kwa sababu amepata, lakini angekosa najua angefunguka tu, yaani huwezi kumfuata mwalimu wako na kumwambia mwalimu umenipatisha….aaaah waaapi!!! hata siku moja. So sisi ndio tuna nafasi kubwa ya kuliona hilo. Nafurahi kuona vitengo na wadau mbalimbali wanajitokeza kuanzisha tuzo zao, kwa ushauri tu ni vema zikaboreshwa zaidi ya hizi zilizopo sasa, ili mabadiliko chanya yaweze kuonekana…Kwa ushauri wangu mchanga ningeweza kuwa – advice wanakamati wajipange kuwa na tuzo nyingi na waongeze categories pia… Kila mtu ana uhuru wa kuongea na kocomment kutokana na hizi tuzo,japo kuwa sio lazima….ila ROMA amezaliwa kukosoa vilivyopinda.
Waliopata tuzo al hamdllh….waliokosa next tym famil-lah ol of ‘em BIG UPS!!!!maisha yanaendelea na mziki unaendelea.....ila ukweli siku zote una tabia ya kushinda…no matter how long will take…..CONSCIOUS FOREVER………….O…N…E”


Habari hii ni maalumu na kwa hisani ya G5 Click.com

Tuesday, May 18, 2010

MWENYEKITI MPYA WA CLUB YA SIMBA AKABIDHIWA OFISI RASMI!!

Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya simba Hassan Dalali mwenye kanzu akimkabidhi nyaraka za uongozi mwenyekiti mpya wa klabu hiyo Ismail Aden Rage.

Saturday, May 15, 2010

MDAU NAMBA 1 WA BLOG HII AKISHOW LOVE!!

Mdau namba 1 wa blog hii ya Easy Men, Ahmed akishow love.mdau anaonekana ni mnazi wa HipHop si unacheki kwenye ze fulanaz yake.

NANI MHUSIKA KUOKOA KITUO HIKI CHA USALAMA WA RAIA!!!

Hiki ni kituo cha Polisi cha kijiji cha Mchukuuni nje kidogo ya jiji la Tanga.ianvyoonekana kituo hiki kimetelekezwa kabisa na hata baadhi ya rasilimali kama Milango na Madirisha kutokuwepo.je wahusika mnataarifa na kituo hiki au ndo kusema maeneo haya Usalama wa Raia na Mali zao ni 100%.!!

BARABARA YA TANGA PANGANI IKIWA KATIKA KIUKARABATI KIDOGO ALASIRI HII!!

Hii ni barabara itokayo Tanga mjini kuelekea wilaya ya Pangani ikiwa katika matengenezo madogo ya kujaza vifusi ili kufukia mashimo mengi yaliyokuwepo kutokana na mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha mkoani Tanga.


SOKO LA NGUO LA KILA JUMAMOSI MAARUFU KAMA TANGAMANO MCHANA WA LEO!!




PARTY IV KILI AWARDS !!!

Wanamuziki wawili kutoka FM academia walikuwepo kushow Love kushoto ni Prezidaa Nyoshi El Sadaat na Mtoto wa Kimara Jose Mara.
Mwanamuziki Marlow akishow love na tuzo yake ya wimbo bora wa Afro Pop.


Mwanamuziki Mrisho Mpoto (Mjomba) akitabasamu baada ya kupokea tuzo ya wimbo bora wa Kiafrika.

Wanamuziki wa Bandi ya African Stars Twanga Pepeta wakiwa pamoja na mkurugenzi mtendaji wa bendi hiyo Baraka Charles aliyeshika tuzo 3 wakifurahi baada ya kupata ushindi mara 3.bendi bora,wimbo bora na rapa bora aliopata Chokoraa.