Thursday, February 17, 2011
VODACOM FOUNDATION KUSAIDIA WAHANGA WA MABOMU YA GONGO LA MBOTO !!!!
Mkurugenzi wa mahusiano na Vodacom Foundation Bi Mwanvita Makamba ameviambia vyombo vya habari kwamba.
Kampuni yake kupitia mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation umeguswa na janga la milipuko ya mabomu yaliyotokea katika kambi ya jeshi ya Gongolamboto jijini Dar es salaam na hivyo kufanya maamuzi ya haraka kama yafuatayo:
1.Kufungua tena namba yao ya maafa ili kuruhusu watanzania ambao wangependa kuchangia wenzao kufanya hivyo kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda 15599 kupitia mitandao yote.Ujumbe huu utatozwa shilingi 1,000 na pesa zote zitaenda kwenye tume ya maafa ya serikali ili kuweza kununua vitu vya dharura vya wahanga.Red alert itawasha kesho Ijumaa tarehe 18.
2.Vodacom Foundation itatoa chakula na vinywaji kwa siku nzima ya Ijumaa kwa wahanga 1000 waliopo uwanja wa Taifa wengi wao wakiwa ni watoto.
3.Pia Vodacom Foundation imetoa namba za simu kwa timu ya Clouds iliyoanzisha kituo cha habari na matukio katika shule ya msingi Mzambarauni Ukonga. Namba hizi zinatumika bure kupiga na kutoa taarifa kama umepotelewa na ndugu au jamaa na pia kutoa taarifa zaidi kuhusu maafa ambayo hayajulikani ili taarifa ziende kwa wahusika.Namba hizo ni 0767111401,0767 111402, 0767 111403.
4.Pampja na kuwawezesha watanzania kutuma michango yao kupitia ujumbe mfupi.Vodacom Foundation pia inakusanya misaada ya chakula na maji na vifaa mbalimbali katika ofisi zao zilizopo Mlimani City kwa watu ambao hawajui waipeleke wapi.Misaada hiyo itakabidhiwa kwa Redcross ambao wanawahudumia wahanga waliopo Uwanja wa Taifa na sehemu mbalimbali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment