Mkurugenzi wa Aurora Security Akitoa shukrani zake mbele ya mkuu wa Mkoa wa Tanga Meja Mstaafu Said Said Kalembo kufuatia kampuni yake ya Aurora kutoa msaada wa Mapipa ya kuhifadhia takataka ambayo yatatumika katika maeneo mbali mbali ya jiji la Tanga. Hafla hii imefanyika katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa serikali na watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga.
Wageni mbalimbali waalikwa katika Uzinduzi huo ambao unaojulikana kama Weka Tanga Safi.
Mapipa ya Kuhifadhia Taka ambayo yametolewa kwa msaada wa Kampuni ya Aurora Security ambayo yatatumika katika maeneo mbali mbali ya jiji la Tanga.
Wageni mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa Idara ya Afya katika Halmashauri ya Jiji la Tanga wakifuatilia kwa makini Uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
Wasanii wa kikundi cha Town Boyz wakitoa burudani katika uzinduzi huo wa weka Tanga Safi leo katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
No comments:
Post a Comment