Sehemu ya wahanga wa Mabomu ya Gongo la Mboto wakiwa ndani ya Uwanja wa Uhuru jijini Dar wakisubiria kujua nini kinaendelea juu yao.
Baadhi ya watoto wakiendelea kuletwa katika uwanja huo wa Uhuru kwa ajili ya mapumziko na kama kuna ndugu aweze kuwatambua.
Wengine walikaa nje ya Uwanja wa Uhuru kupumzika na kupata vivuli vya miti kutokana na kutolala usiku wa kuamkia leo kwa hali ya milipuko ya mabomu iliyotokea maeneo ya Gongo la Mboto katika maghala ya silaha ndani ya kambi ya jeshi la wananchi (JWTZ)
Mtoto Gerald Samson ambaye ni mmoja wa wahanga akiwa na majeraha usoni mara baada ya kuumia wakati akijaribu kutaka kujinusuru na milipuko hiyo jana usiku.
Hawa ni watoto waliookotwa huko Gongo la Mboto wakiwa peke yao kutokana na wazazi wao kukimbilia sehemu zisizojulikana kutokana na mabomu yaliyokuwa yakilipuka usiku wa kuamkia leo katika kambi ya jeshi la wananchi (JWTZ)huko Gongo la mboto.
Bw Salum Madaba wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa pamoja na mwalimu Kiondo kutoka shule ya msingi Tandika wakimnywesha maziwa mmoja wa watoto waliopo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar.ambapo haikufahamika wazazi wake wapo wapi mpaka leo hii.
Afisa Msalaba Mwekundu mama Jane Lweikiza akiwa amembeba mtoto aliyekutwa maeneo ya Sitaki Shari Ukonga mchana huu kutokana na kutojulikana walipo wazazi wake mara baada ya kutokea kwa milipuko ya mabomu katika kambi ya jeshi la Wananchi (JWTZ) Gongo la mboto usiku wa kuamkia leo.
Watu wa msalaba mwekundu wakishusha maji ya kunywa kwa ajili ya wahanga hao waliopo ndani ya uwanja wa Uhuru jijini Dar,