Thursday, December 2, 2010
WAZIRI MAGUFULI AMTIMUA KAZI CEO WA TANROADS !!
Waziri wa ujenzi Dk John Magufuli ameanza kazi kwa maamuzi magumu kwa kumfukuza kazi mtendaji mkuu(CEO)wa wakala wa barabara Tanzania(TANROAD)Ndg Ephraim Mrema.
Habari za uhakika ambazo Nipashe limezipata kutoka vyanzo vya kuaminika zianaeleza kwamba Magufuli alifanya uamuzi huo jana.
Vyanzo hivyo havikueleza sababu ya kumtimua mrema zaidi ya kusema uamuzi huo unaanza mara moja.
Habari zaidi zinasema kuwa Dk Magufuli alimtaka Mrema kukabidhi ofisi jana mchana na nafasi yake inashikiliwa kwa muda na mkurugenzi wa barabara za vijijini Patrik Mfugale.
Hata hivyo Nipashe lilimtafuta Dk Magufuli jana usiku ili kuthibisha uamuzi huo lakini simu yake ya kiganjani ilikuwa imezimwa.habari kwa hisani ya nipashe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment