Friday, December 31, 2010
MH.UMMY ATEMBELEA TUJIKOMBOE GROUP TANGA!!!
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Bi.Ummy Ally Mwalimu kulia akipokea risala kutoka kwa Mwasisi Mshauri wa Shirika lisilo la kiserikali la Tujikomboe Group Bw.Shamsi Mhina ,Shirika hilo lenye makao yake Ngamiani Kusini Tanga linalojishughulisha na masuala ya kutetea haki za watoto,Maendeleo ya Jamii(Picha na Benedict Kaguo)
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Bi.Ummy Ally Mwalimu (katikati asiye na kilemba) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Tujikomboe Group alipowatembelea jana,kulia ni Bw.Shamshi Mhina Mwasisi na Mshauri wa Shirika hilo,kushoto ni Bi Chiku Athumani Mratibu wa Shirika hilo Tanga,walioko nyuma ni Afisa Tawala Bi.Mariam Amiri na Mwanaisha Issa Msaidizi wa Ofisi,Naibu Waziri alitembelea kujua shughuli za asasi hiyo(Picha na Benedict Kaguo)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment