Waliosimama..Remmy Ongala, Abuu Semhando, Kasaloo Kyanga, Fan FanRatiba ya Mazishi ya mwanamuziki na na meneja wa Bendi ya African Stars-Twanga Pepeta Marehemu Abou Ally Semhando “Baba Diana”· Jumamosi ndugu na jamaa walikusanyika nyumbani kwa marehemu, Mwananyamala Kisiwani(Ngilangwa) kwa ajili ya kutoa pole na kuwafariji wafiwa.
· Leo Jumapili 19/12-Saa11 baada ya Swala ya alfajiri katika msikiti wa Muhimbili, waombolezaji kuingia katika magari na kuelekea kijiji cha Kibanda, Muheza tayari kwa mazishi.
· Mara baada ya chakula cha mchana mwili kupelekwa msikiti wa Muheza nabaada ya swala mwili kupelekwa makaburini kwa maziko.
· Waombolezaji watarejea Dar es Salaam baada ya maziko.
Hakika Msiba wa Abou unaumiza sana
1. Jumamosi ni siku aliyokuwa amuoze binti yake wa kwanza
2. Alikuwa ameuandikia uongozi wa Bendi kuwa umpe likizo ya mwezi kwani alitaka asiweko katika jukwaa kwa kipindi. Ni mara ya kwanza yeye kuandika barua ya kuomba likizo
3. Katika simu yake ringtone aliyoiweka ni ya wimbo wa Njohole Jazz Band- bendi hii wanamuziki wake karibu wote walikufa pamoja katika ajali mbaya ya gari.
4. Alikuwa mpiga drum wa Dk. Remmy Ongala enzi za Super Matimila na mtindo wao wa Talakaka mwaka 1981
-John Kitime