Wizara ya viwanda biashara na masoko imesema iko katika mchakato wa kukamilisha muswada ya mabadiliko ya sheria ya hatimiliki na haki shiriki ili kudhibiti wizi wa kazi za wasanii nchini.
Akizungumza mwishoni mwa wiki kwa njia ya simu,waziri wa wizara hiyo Cyril Chami (pichani)alisisitiza kwamab serikali inatambua kilio cah wasanii juu ya uboreshwaji wa sheria ya Hatimiliki na hakishiriki ya mwaka 1999 na kwamba jitihada zinafanyika kufanikisha marekebisho hayo.
Wizara inatambua kilio cha wasanii na inajali maslahi.wasanii ni kundi muhimu na tunalipa umuhimu na umakini unaostahili,kazi zao zinahitaji kulindwa na kuheshimiwa,na kumekuwa na jitihada kuhakikisha hilo linafanyika,alisema Chami.
Waziri Chami alibainisha kwamba kuchelewa kupitishwa ka muswada huo,kunatokana na tofauti zilizopo kati ya makundi mawili ya wasanii,lile la muziki na wa fani nyinginezo,ambazo zitajadiliwa katika kikao baina ya wizara mbili.
Wizara hizo ni ile ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo na ile ya Viwanda, biashara na masoko.
No comments:
Post a Comment