SIKILIZA NYIMBO ZA EASYMEN HAPA:


Electronic Press Kit
Quantcast

Tazama Small Interview ya Easymen Studio Hapa:

Friday, April 8, 2011

LEO MAJIRA YA 6 MCHANA KULITOKEA AJALI MBAYA YA BASI DOGO LA ABIRIA NA MWENDESHA PIKIPIKI KATIKATI YA JIJI LA TANGA !!!!

Leo majira ya saa 6 mchana katika barabara ya Taifa Road ( Barabara ya 4 - Tawakal )jijini Tanga kulitokea ajali mbaya sana iliyohusisha daladala moja linalofanya safari kati ya Donge - Raskazone na mwendesha pikipiki.chanzo cha ajali hii inasemekana ni muendesha pikipiki kukatiza barabara ghafla wakati akitaka kuwakwepa Askari wa usalama barabarani ili arudi alipotoka lakini daladala hiyo ilikuwa karibu sana na kumgonga vibaya sana.Mashuhuda wa ajali wanasema mendesha pikipiki huyo alivunjika miguu yote miwil hapohapo na hali yake ni mbaya na amekimbizwa Hospital.
Pichani ni pikipiki hiyo ikiwa chini ya uvungu wa daladala hilo.

Wananchi mbalimbali wakiangalia askari wakiendelea kupima ajali hiyo.

Wananchi mbalimbali wakiangalia ajali hiyo iliyohusisha basi dogo la abiria daladala na mwendesha pikipiki katika eneo la Tawakal barabara ya 4 jijini Tanga.

Pichani pikipiki hiyo ikiwa chini ya uvungu wa basi dogo la daladala linalofanya safari kati ya DONGE - RASKAZONE jijini Tanga.

No comments:

Post a Comment