SIKILIZA NYIMBO ZA EASYMEN HAPA:


Electronic Press Kit
Quantcast

Tazama Small Interview ya Easymen Studio Hapa:

Saturday, April 30, 2011

TAMASHA LA TIGO PESA KATIKA VIWANJA VYA TANGAMANO JIJINI TANGA LEO !!!


Wasanii chipukizi toka Tanga wakitumbuiza Jukwaani.Pia katika tamasha hili wasanii mbalimbali toka Dar walikonga nyoyo za wanachi wakiwemo TMK WANAUME wakiongozwa na Juma Nature,AFANDE SELE,ROMA, 20 PERCENT.

Wakazi mbalimbali wa jiji la Tanga walijitokeza kushuhudia Tamasha hilo la Tigo Pesa lililofanyika katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga.

Watu mbalimbali wakishuhudia Tamasha hilo.

MAANDALIZI YA SAFARI YETU YA VIJANA KWENDA NCHINI HUNGARY KWA MIEZI 2 !!!


Vijana 10 wanachama wa kituo cha vijana Nguvumali Tanga.tukiwa katika ofisi zetu za kituo kujaza fomu za maombi ya Hati za Kusafiria kwa ajili ya kujiandaa na safari yetu itakayochukua miezi 2 nchini HUNGARY kutoka mwezi June 2011.Safari hii ina malengo ya kubadilishana uzoefu kati ya vijana wa nchini HUNGARY katika mji wa PECS na vijana wa TANZANIA katika jiji la Tanga.


Tukiwa nje ya ofisi ya Uhamiaji mkoa wa Tanga kufanya uhakiki wa mwisho wa fomu hizo kabla ya kuzikabidhi katika Ofisi hizo za Uhamiaji.tunashukuru sana maafisa uhamiaji mkoa wa Tanga kwa kutusaidia kwa moyo wa upendo.sasa tunasubiri maganda tu ili hatua nyingine ifuate haraka.

Wednesday, April 27, 2011

RAMSEY ATUA JIJINI DAR KUREKODI FILAMU NA WASANII WA BONGO !!!


Ramsey(kushoto)akiwa na nguli wa Filamu nchini Steven Kanumba wakizungumza na waandishi wa habari juu ya filamu hiyo.
Msanii maarufu wa Filamu toka Nigeria Ramsey Tokumbo Nouah ametinga nchini kurekodi filamu na wasanii mbalimbali wa Tanzania akiwemo Steven Kanumba.akizungumza na waandishi wa habari jana mchana katika Hotel ya Peacok jijini Dar,Ramsey amesema Filamu hiyo itakuwa ya aina yake.

Friday, April 22, 2011

OPERESHENI VUA GAMBA YA CCM YAHAMIA IRINGA !!!


Nape Nnauye na John Chiligati wakiwa na baadhi ya wanachama wa CCM

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, John Chiligati (katikati) akiwa na viongozi na wanachama wa CCM Mkoa wa Iringa, baada ya kumaliza mkutano wa hadhara kwa ajili ya oparesheni ya 'Vua Gamba' uliofanyika mjini Iringa jana. Wa pili kushoto ni Kamanda wa Vijana wa CCM, Mkoa wa Iringa, Salim

BALOZI WA UINGEREZA NCHINI AMTEMBELEA DK SHEIN IKULU ZANZIBAR !!!


Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,akimsindikiza Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,Dianne Corner, Ikulu Mjini Zanzibar jana,baada ya mazungumzo yao.


Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,akimsindikiza Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,Dianne Corner, Ikulu Mjini Zanzibar jana,baada ya mazungumzo yao.

Wednesday, April 20, 2011

WIZARA KUKAMILISHA MUSWADA WA HATIMILIKI NA HAKISHIRIKI !!


Wizara ya viwanda biashara na masoko imesema iko katika mchakato wa kukamilisha muswada ya mabadiliko ya sheria ya hatimiliki na haki shiriki ili kudhibiti wizi wa kazi za wasanii nchini.
Akizungumza mwishoni mwa wiki kwa njia ya simu,waziri wa wizara hiyo Cyril Chami (pichani)alisisitiza kwamab serikali inatambua kilio cah wasanii juu ya uboreshwaji wa sheria ya Hatimiliki na hakishiriki ya mwaka 1999 na kwamba jitihada zinafanyika kufanikisha marekebisho hayo.
Wizara inatambua kilio cha wasanii na inajali maslahi.wasanii ni kundi muhimu na tunalipa umuhimu na umakini unaostahili,kazi zao zinahitaji kulindwa na kuheshimiwa,na kumekuwa na jitihada kuhakikisha hilo linafanyika,alisema Chami.
Waziri Chami alibainisha kwamba kuchelewa kupitishwa ka muswada huo,kunatokana na tofauti zilizopo kati ya makundi mawili ya wasanii,lile la muziki na wa fani nyinginezo,ambazo zitajadiliwa katika kikao baina ya wizara mbili.
Wizara hizo ni ile ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo na ile ya Viwanda, biashara na masoko.

Thursday, April 14, 2011

TWIGA STARS WAKIWA MAZOEZINI LEO !!!


Wachezaji wa timu soka ya Taifa ya wanawake "Twiga Stars" wakifanya mazoezi leo asubuhi kwenye uwanja wa Karume,Dar es Salaam.ikiwa ni maandalizi ya timu hiyo kwa ajili ya michuano ya awali ya kusaka tiketi ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika.Picha toka Michuzi Blog.

Wednesday, April 13, 2011

KAGAME CUP KUFANYIKA SUDAN KUANZIA JUNE 21 HADI JULAI 5 !!!!


Rais wa RWANDA KAGAME akiwa na katibu mkuu wa CECAFA MUSONYE.
Michuano ya kombe la KAGAME inatalajiwa kuanza kutimua vumbi june 21 mpaka Julai 5 ambapo timu zitakzoshiriki mashindano hayo zinatakiwa kuthibitisha hadi kufikia April 30 mwaka huu.


Kwa mujibu wa barua kutoka kwa katibu mkuu wa CECAFA NICHOLAS MUSONYE anasema katika mashindano hayo timu ya MISRI itashiriki kama mwalikwa .

KUANZISHWA KWA CHAMA CHA KITAALAM CHA WAPISHI TANZANIA !!!


TAARIFA NJEMA KWA WAPISHI WOTE WA KITANZANIA.
Active chefs Association of Tanzania (acat 2011)


BAADA YA MAFANIKIO MAKUBWA YA BLOG YA ACTIVECHEF SASA NIMEAMUA KUANZISHA CHAMA CHA KITAALAMU CHA WAPISHI TANZANIA. CHAMA HIKI NI CHAMA KISICHO CHA KIBIASHARA.


NATOA WITO KWA NDUGU ZANGU WATANZANIA WAPISHI WA HAPA NYUMBANI NA WALIOKO NJE YA NCHI TUUNGANE NA TUJENGE CHAMA CHENYE NGUVU TUWEZE TAMBULIKA KATIKA ULIMWENGU WA MAPISHI DUNIANI.


KWASASA TAYARI WAMESHAPATIKANA WANACHAMA KUMI WATANZANIA TOKA SAUDI ARABIA, AMERICA, SWISS NA UK. NAWAKARIBISHA WOTE MJIUNGE NI BURE HAKUNA ADA YEYOTE. FOMU ZA KUJIUNGA TUMA EMAIL issakesu@gmail.com KISHA NITAKUATUMIA HARAKA NAWE UNAJAZ ANA KUSCAN KISHA UNANITUMIA. KUANZIA MWEZI UJAO TUTAKUA NA WEBSITE YA CHAMA NA EMAIL YA CHAMA IPO KATIKA MATENGENEZO.

Friday, April 8, 2011

MWENYEKITI WA CHADEMA MBEYA AJIUNGA CCM,RAIS KIKWETE AMPA KADI YA CCM MJINI DODOMA LEO !!!



Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akinyanyua mikono ya viongozi waandamizi wa Chadema mkoa wa Mbeya waliokihama chama hicho rasmi na kuhamia CCM mjini Dodoma leo mchana. Kushoto ni aliyekuwa katibu wa CHADEMA wilaya ya Ileje Henry Rafael Kayuni na kulia ni aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya Bw Shambwee Shitambala.kulia ni waziri wa maji ambaye pia ni mjube wa NEC,CCM Mkoa wa Mbeya Prof Mark Mwandosya



Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt Jakaya Kikwete akimpongeza aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya Bw Shamwee Shitamabala muda mfupi baada ya kupokea kadi ya CCM mjini Dodoma leo mchana.



Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi kadi ya kujiunga na chama cha Mapinduzi aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya.wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha CCM baada ya kukihama rasmi CHADEMA katika makao makuu ya CCM mjini Dodoma leo Mchana.

KUTOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA LEO IMENILAZIMU KUFUFUA GARI YA OFISI ILI NIWEZE KUDUNDA MITAANI BILA YA KUHOFIA MVUA !!!



Pichani ni gari ambayo huwa mara nyingi naitumia kwa shughuli za ofisi ili kuweza kurahisisha mizunguko.leo ilinilazimu kutafuta mafundi wa kulifufua ili nianze kulitumia tena kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini hapa na bila kipando kama hiki shughuli zitakwama.



Pichani fundi akiendelea kulifanyia matengenezo.

LEO TULIPATA WAGENI KATIKA OFISI YETU YA KITUO CHA VIJANA NGUVUMALI JIJINI TANGA !!!


Hapa ni picha ya pamoja kati ya vijana wanachama wa kituo cha vijana Nguvumali jijini Tanga tukiwa katika picha ya pamoja na wageni waliotutembelea kuona kituo chetu pamoja na Studio yetu kubwa ya Kurekodi muziki inayojulikana kama 2MORROW RECORDZ.

LEO MAJIRA YA 6 MCHANA KULITOKEA AJALI MBAYA YA BASI DOGO LA ABIRIA NA MWENDESHA PIKIPIKI KATIKATI YA JIJI LA TANGA !!!!

Leo majira ya saa 6 mchana katika barabara ya Taifa Road ( Barabara ya 4 - Tawakal )jijini Tanga kulitokea ajali mbaya sana iliyohusisha daladala moja linalofanya safari kati ya Donge - Raskazone na mwendesha pikipiki.chanzo cha ajali hii inasemekana ni muendesha pikipiki kukatiza barabara ghafla wakati akitaka kuwakwepa Askari wa usalama barabarani ili arudi alipotoka lakini daladala hiyo ilikuwa karibu sana na kumgonga vibaya sana.Mashuhuda wa ajali wanasema mendesha pikipiki huyo alivunjika miguu yote miwil hapohapo na hali yake ni mbaya na amekimbizwa Hospital.
Pichani ni pikipiki hiyo ikiwa chini ya uvungu wa daladala hilo.

Wananchi mbalimbali wakiangalia askari wakiendelea kupima ajali hiyo.

Wananchi mbalimbali wakiangalia ajali hiyo iliyohusisha basi dogo la abiria daladala na mwendesha pikipiki katika eneo la Tawakal barabara ya 4 jijini Tanga.

Pichani pikipiki hiyo ikiwa chini ya uvungu wa basi dogo la daladala linalofanya safari kati ya DONGE - RASKAZONE jijini Tanga.

Thursday, April 7, 2011

NIKIWA NA RAFIKI TOKA NORWAY !!!!


Mimi Pashua nikiwa na rafiki tukipata picha ya ukumbusho.

Saturday, April 2, 2011

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BUNGE!!!


Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
--


Katibu wa Bunge anautangazia umma kuwa, Mkutano wa Tatu wa Bunge la Kumi utaanza tarehe 5 Aprili, 2011 Mjini Dodoma.






Imetolewa na:


Idara ya Habari, Elimu kwa Umma


na Uhusiano wa Kimataifa


DAR ES SALAAM


1 Aprili, 2011

LEO NI SIKU YA KUWAPONGEZA WALIOPATA TUZO ZA KTMA , 20% NA MAPACHA 3 NDANI YA MZALENDO PUB!!!