Wednesday, September 22, 2010
MWAKALEBELA ATIKISA IRINGA.AKUBALI YAISHE NA KUYAZIKA MAKUNDI !!
Mgombea Urais wa chama cha CCM,Mh Jakaya Kikwete akiwa na Frederick Mwakalebela kwa pamoja wakiwasalimia wananchi waliofika kwenye mkutano wa kampeni za chama hicho uliofanyika leo mjini Iringa
Wwwoooowww..!
Mgombea Urais chama cha CCM,Mh Jakaya Kikwete na Frederick Mwakalebela.
================
Frederick Mwakalebela ashangiliwa kuliko mgombea urais wa CCM, jazba ya wana Iringa dhidi ya kutemwa kwa kwake yaonyeshwa mbele ya Jakaya Kikwete, yeye aamua kupanda naye jukwaani .
Hata hivyo CCM jimbo la Iringa mjini imeweza kutumia jukwaa hilo la mgombea Urais kwa kuwataka wagombea wote walioshiriki katika kinyang’anyiro cha kura za maoni kupanda jukwaani ili kuvunja makundi huku wote wakikosa kushangiliwa zaidi ya Mwakalebela aliyeonyesha kushangiliwa kwa nguvu zote kuliko hata burudani zilizokuwepo hapo na wagombea wenzake.
Akitangaza kuvunja makundi ya kura za maoni Mwakalebela alisema kuwa kwa sasa ataelekeza nguvu zake zote kwa Mbega kama mgombea ubunge wa jimbo hilo na madiwani wote wa CCM na mgombea huyu wa urais Dr.Kikwete na kuwataka wapinzani wasimtumie kama sera zao.Picha zote kwa hisani ya Francis Godwin kutoka Iringa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment