Friday, September 10, 2010
MGOMBEA URAIS WA CCM DR JAKAYA KIKWETE ATOA MKONO WA EIDD KWA WAISLAM MKOANI TANGA!!
Mgombea Urais kwa chama cha CCM,Mh Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu muda mfupi baada ya kumalizika kwa swalla ya Iddi iliyoswaliwa katika Msikiti Mkuu wa Riyadh mjini Tanga leo asubuhi
Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Mufti Mkuu sheikh Issa Shaaban Simba wakati wa Swalla ya Iddi iliyoswaliwa mjini Tanga leo.Katikati anayeangalia ni Mgombea Urais kwa chama cha CCM,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete
Mgombea Urais kwa chama CCM,Mh Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono wa Iddi na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi wakati wa Swalla ya Iddi iliyoswaliwa katika Msikiti mkuu wa Riyadh mjini Tanga.Mzee Mwinyi ndiye mgeni Rasmi katika baraza la Iddi litakalofanyika kitaifa mjini Tanga.
Mgombea Urais kwa chama cha CCM,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaaban Simba wakati wa swalla ya Idd iliyoswaliwa kwenye Msikiti Mkuu wa Riyadh mjini Tanga leo asubuhi (picha na Freddy Maro)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment