Kocha Mkuu wa Timu ya Simba Phiri akishow love kwa mashabiki wakati wa kuondoka uwanjani
Kocha wa Timu ya Taifa Jan Paulsen akiwa kwenye iliyomleta uwanjani pamoja na Afisa habari wa TFF Florian Kaijage.
K ocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania Jan Paulsen akishow Love ndani ya Kamera ya blog hii ya Easymen ndani ya Uwanja wa Mkwakwani.
Afisa habari wa TFF Florian Kaijage akiondoka uwanjani baada ya Mchezo baina ya Simba na Azam kuisha.
Basi la Wachezaji wa Azam Fc likiwa limepark tayari kwa safari ya kurudi Dar es Salaam baaday ya mchezo wao na Simba katika Hotel ya Central City barabara 8 jijini Tanga ambapo ndipo wachezaji hao walipofikia.
Mashabiki wa Timu ya Simba wa jijini Tanga wakimpa hongera mtoto wa Home Uhuru Suleiman akiwa kwenye gari baada ya Mechi kumalizika.
Mchezaji wa Simba akishow love na mashabiki wa Timu hiyo wakati wakitoka Uwanjani.
Basi la wachezaji wa Timu ya Azam Ndani ya Uwanja wa Mkwakwani punde tu baada ya Mechi kumalizika na Simba kutoka kifua mbele kwa Goli 2 - 1.
Basi la mashabiki wa Simba toka Dar es salaam likiondoka ndani ya Uwanja wa Mkwakwani kwa mbwembwe baada ya kupata ushindi dhidi ya Azam Fc.
Baadhi ya Mashabiki waliamua Kuingia uwanjani kupitia ukutani kutokana na Ticket za Mchezo huo kuisha mapema na uwanja kujaa na Kufungwa mida ya Saa kumi na nusu jioni.
Hii pia ilikuwa ni njia ya Kuingia uwanjani baada ya kuwa Ticket zimekwisha mapema na uwanja kufungwa.amabpo inasemekana Ticket zilitengenezwa 14,000 zote ziliisha.
Baadhi ya Mashabiki wa Azam waliotoka Dar es Salaam wakifanya vurugu mlango mkuu wa Uwanja wa Mkwakwani baada ya kuambiwa kuwa Ticket zimekwisha na hawataweza kuingia na kuona mchezo huo.
Mashabiki wengi waliotoka mikoani na wa jijini Tanga hawakuweza kuona mchezo huu kutokana na Ticket kuwa kidogo na Uwanja kujaa.hata mimi mwandishi wa Blog hii nilifika Uwanjani Saa kumi na dakika tano pamoja rafiki zangu lakini hatukuweza kuingia na kuona mchezo huu.