Kila ifikapo tarehe 1 July ni siku ya maadhimisho ya Serikali za mitaa Nchini.Katika Jiji la Tanga hali ilikuwa tofauti ambapo Wenyeviti wa mitaa 141 kati ya 146 wa jiji hili walisusia kufanya maandamano ya Kuadhimisha siku hiyo katika jiji hili la Tanga,ambapo sherehe hizo zilifanyika katika Viwanja vya Uhuru Park na kuhudhuriwa na wenyeviti 5 tu kati ya 146 wa jiji hili.
Wenyeviti hao 141 walifanya mgomo huo kutokana na kuwa na kero mbalimbali zinazowakabili zikiwemo Halmashauri ya Jiji la Tanga kuto wajali na kuwadharau katika kuwatatulia matatizo yao ambayo ni kutoshirikishwa katika shughuli mbalimbali za maendeleo,Kutopata vitambulisho rasmi vya kutambulika kama wenyeviti wa Mitaa,Kukosa mihuri rasmi,Karatasi,Bendera za utambulisho,Ofisi za kuwahudumia wananchi ambapo kwa sasa inabidi wananchi wawafuate majumbani kwao.Posho ndogo nk.
Aidha katika maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na Madiwani,watendaji wa kata pamoja na watumishi mbalimbali wa Serikali na wananchi kwa ujumla yalileta hamasa kubwa baada ya Mgeni rasmi ambaye ni Naibu Meya wa jiji la Tanga kuuliza mbona watendaji ni kidogo alijibiwa Wamegoma.na naibu meya huyo kuahidi kushughulikia suala hilo baadae.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment