Timu ya Vijana wadogo ya mpira wa miguu ya Mkoa wa Tanga iliyokuwa ikishiriki kwenye Fainali za Copa CocaCola zilizokuwa zinaendelea jijini Dar es Salaam imefungiwa kuendelea na Mashindano hayo huku Viongozi wa Timu hiyo kufungiwa Kushiriki katika Shughuli za Kisoka kwa muda kati ya miezi 6 hadi miaka 2.
Hatua hiyo imechukuliwa na Shirikisho la Michezo wa Kandanda Tanzania TFF jana jioni baada ya Kubaini kuwa na udanganyifu wa Umri pamoja na kughushi majina kwa wachezaji 2 wa timu hiyo ya Tanga.
Awali Timu hiyo ya Mkoa wa Tanga ilikuwa inashikilia nafasi ya Pili ambayo ilitakiwa kucheza nusu fainali na badala yake nafasi hiyo inachukuliwa na timu ya mkoa wa Mbeya.
Kwa upande wa wadu wa michezo wa Mkoa wa Tanga wamesikitishwa kwa hatua hiyo iliyochukuliwa lakini pia kwa upande mwengine Viongozi wa mchezo huo kwa mkoa wa Tanga watajifunza kutokana na vitendo vyao viovu mbele ya Tasnia ya Michezo na Mkoa kwa Ujumla.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment