Hili ni baadhi ya Mabango waliyokuwa wamebeba wazee hao likiandikwa Kalembo mkombozi wa Tanga.
Na hili pia ni moja ya bango katika maandano hayo likiandikwa tunataka viongozi waadilifu.
Na hili linasomeka lenyewe jamani.!!
Hapa ni baadhi ya waandamanaji wakijiandaa kuingia katika viwanja vya Tangamano ambapo ndio palikuwa na mkutano wa Hadhara ulioitishwa na wazee hao wa jiji la Tanga.maandamano hayo yalianzia katika viwanja vya Garden na kupita katika barabara zote za jiji la Tanga yaani bar 1 hadi 21 na kisha kuishia katika viwanja vya Tangamano.
Hapa ni gari ya Mgeni rasmi ambaye alipokea maandamano hayo pamoja na risala ya wazee wa jiji la Tanga.si mwingine bali ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Dk,Ibrahimu Msengi amabaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa.
Pichani ni msoma risala wa siku hiyo.amabapo katika risala hiyo wazee wa jiji la Tanga walimuomba Mkuu wa Mkoa wa Tanga kuendelea na msimamo wake huo wa kuwasimamisha kazi viongozi hao,ikiwa ni pamoja na kutoa kero mbalimbali zinazoikabili jiji la Tanga ikiwemo; barabara zinazojengwa chini ya kiwango,taa za barabarani zisizowaka, kukithiri kwa vitendo vya Rushwa katika halmashauri ya jiji la Tanga,Ubadhirifu wa fedha za Mradi wa Tasaf, ucheleweshwaji wa makusudi wa ujenzi wa Hospitali ya wilaya ambayo iliafikiwa ijengwe maeneo ya masiwani jijini Tanga. lakini pia walimuomba mkuu wa Mkoa kumweleza Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete kuchukua hatua za Haraka kuvunja baraza la madiwani la Jiji la Tanga ambalo limekuwa likiwakingia kifua Mkurugenzi asisimamishwe kazi kwani Mkuu wa Mkoa hana mamlaka ya kufanya hivyo.hivyo kutokana na hali hiyo wazee wa jiji la Tanga hawana imani na baraza hilo la madiwani na kuamini labda kuna ushirikiano katika utendaji wa maovu katika halmashauri hiyo.
No comments:
Post a Comment