Juzi siku ya Ahamisi nilifika Internent Cafe moja katikati ya Jiji la Tanga na kausafiri kangu ka baiskeli ya kukodi ili kuwahi add news.nilipark Baiskeli nje na kuingia ndani.lakini wakati nipo katika harakati za kutafuta park ya kaibaskeli kangu nje ya Cafe walipita vijana wawili waliokuwa wamepakizana kwenye baiskeli yao na wakaelekea mitaa ya mbele.
Sasa wakati nipo ndani naendelea kubrowse mara akaingia kijana yule mmoja wao kati ya wale wawili waliokuwa wamepita kwa nje.alipoingia ndani akamuuliza muhudumu wa Cafe kwamba anamuulizia dada mmoja anaitwa Sauda anafanya kazi za kompyuta.
Sasa mimi baada ya kumuona yule kijana machale yalinicheza nikanyanyuka kidogo kuangalia kausafiri kangu kwa nje nilikokapaki kako salama ile kuangalia nikaona tairi ya kausafiri kangu inaondoka taratibu,basi mimi nikaacha kubrowse haraka sana nikaanza kumfukuzia aliyekuwa anaiba kausafiri kangu.nilipofika nje nilimuona anamalizikia kwenye kona sikuweza kumpata.lakini nilishajua kabisa kwamba kila ilivyo huyu kijana aliyekuwa ndani Cafe akiuliza yule aliyekwiba kausafiri kangu ni yule mwenzake aliyekuwa amempakia kwenye baiskeli kabla ya mimi Kuingia Cafe.basi alipotoka Cafe na kutaka kupanda baiskeli yake aondoke mimi nilimkamata na kuanza kumchapa kidogo aseme yule mwenzie ni nani na anakaa wapi kwa maana mchezo wao wote nilishaustukia.basi baada ya kipondo kidogo alikri yule ni mwenzie ila afahamu anapokaa.mimi nikamwambia sasa nachukua hii baiskeli yako mpaka umfate mwenzio mrudishe ya kwangu na nitakupeni ya kwenu.
sasa karibu kabisa na hiyo Cafe kuna Askari wanaolinda benki ya Exim Bank, nikamwambia twende nikupeleke pale na mimi niiache hii baiskeli yako kwa wale askari ukamfate mwenzio mrudishe baiskeli yangu na niwape ya kwenu.na nikamwambia ukibisha nakupigia kelele za mwizi basi akatii amri,wakati tunaelekea kwa hao askari baada ya kama hatua tano alinipochoka na kutimua mbio na kuniachia Baiskeli yake.
Sasa nilikwenda kituo cha Polisi na kutoa taarifa na kunipatia RB No:TAN/RB/3397/10.na polisi kuniambia niiache hiyo baiskeli kwa siku 3 kama hawakutokea kurudisha ya kwangu nichukue hii iwe mali yangu. lakini hoja ni kwamba hii baiskeli waliyokimbia na kuniachia imeandikwa BLACK FIGHTER No:5 kama inavyoonekana hapo juu.inaonekana ni ya kukodi pia.
Sasa msaada ninaohitaji kama kuna mtu yeyote anayefahamu mahali Tanga hii kuna baiskeli zinakokodishwa zimeandikwa jina hilo hapo juu anipe taarifa ili niweze kufatilia.
Contact zangu zipo hapo juu kwenye profile Picture yangu.
Ahsanteni
Wenu Pashua.
No comments:
Post a Comment