SIKILIZA NYIMBO ZA EASYMEN HAPA:


Electronic Press Kit
Quantcast

Tazama Small Interview ya Easymen Studio Hapa:

Saturday, June 26, 2010

MWANAMUZIKI JOSEPH MBILINYI MAARUFU KAMA MR II PROUD (SUGU) AJIUNGA NA RASMI NA CHAMA CHA CHADEMA !!

Pichani katika ni Mwanamuziki muasisi wa Bongo fleva nchini Mr 2 (Sugu) akionyesha kitambulisho kwa kutambulika rasmi kuwa mwanachama wa chama cha Chadema.Kushoto kwake ni Bw John Mnyika wa Chadema aliyemkabidhi Mr 2 Kitambulisho hicho.
Mr 2 amekuwa mwanamuziki wa pili hapa nchini kutangaza rasmi nia ya kujiunga na chama Demokrasia na maendeleo CHADEMA.Wakati wa kwanza kufanya hivyo ni mwanamuziki wa kike maarufu kama Nakaaya Sumari.

Tuesday, June 22, 2010

HATIMAYE MNYANGE WA KUIWAKILISHA TANGA APATIKANA !!!

Mnyange wa Miss Tanga 2010 Anna Kiwambo akiwa katika uso wa furaha punde tu baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika mchakato huo uliofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort iliyopo Sahare, Miss Tanga 2010 imeandaliwa na 5 Brothers Entertainment.
Pichani ni Aziza Khalifa ambaye pia ni Miss Pangani 2010 alipotangazwa kuwa mnyange wa Miss Talent Tanga 2010. Miss Pangani 2010 iliandaliwa na Anko Mo Blogspot.

Anna Kiwambo akiwa na washindi wengine, mshindi wa pili alikuwa ni Jari Mure, wa tatu ni Zuleha Mrisho. Nafasi ya nne alichukua Asia Gumbo na nafasi ya tano alinyakua Grace Joseph.


Tano Bora ya Miss Tanga 2010.


Mkuu wa mkoa wa Tanga Saidi Kalembo akimpa mkono wa hongera mnyange wa Miss Tanga 2010.




Msanii mahiri wa Bongo Flava kutokea Tanga Matonya, aki'show Love kwa Miss Tanga 2010.





Mrembo aliyekuwa anamaliza muda wake Glory Chuwa ambaye ni Miss Tanga 2009 akiwa katika tabasamu nono.






Majaji wakiwa makini na kazi yao.







Chifu jaji Musa Kisoki alikuwa na kazi ngumu ya kutangaza mshindi.
Kisoki ni mkurugenzi wa kampuni ya Sofia Production








Sunday, June 20, 2010

SIKU YA JANA JUMAMOSI TAR 19 JUNE.WAZEE WA JIJI LA TANGA WALIFANYA MAANDAMANO YA AMANI KUMUUNGA MKONO MKUU WA MKOA WA TANGA.!!!!

Pichani ni maandamano ya amani yalioandaliwa na wazee wa jiji la Tanga kumuunga Mkono Mkuu wa mkoa wa Tanga Mej,Mstaafu Said Said Kalembo kufuatia uamuzi wa kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa jiji la Tanga na Mhandisi.baada ya kugundulika kuwa kuna mazingira ya Rushwa katika utoaji wa Tenda ya Ujenzi wa Barabara ya Bombo, Raskazone.
Hili ni baadhi ya Mabango waliyokuwa wamebeba wazee hao likiandikwa Kalembo mkombozi wa Tanga.




Na hili pia ni moja ya bango katika maandano hayo likiandikwa tunataka viongozi waadilifu.



Na hili linasomeka lenyewe jamani.!!


Hapa ni baadhi ya waandamanaji wakijiandaa kuingia katika viwanja vya Tangamano ambapo ndio palikuwa na mkutano wa Hadhara ulioitishwa na wazee hao wa jiji la Tanga.maandamano hayo yalianzia katika viwanja vya Garden na kupita katika barabara zote za jiji la Tanga yaani bar 1 hadi 21 na kisha kuishia katika viwanja vya Tangamano.


Hapa ni gari ya Mgeni rasmi ambaye alipokea maandamano hayo pamoja na risala ya wazee wa jiji la Tanga.si mwingine bali ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Dk,Ibrahimu Msengi amabaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa.







Pichani ni msoma risala wa siku hiyo.amabapo katika risala hiyo wazee wa jiji la Tanga walimuomba Mkuu wa Mkoa wa Tanga kuendelea na msimamo wake huo wa kuwasimamisha kazi viongozi hao,ikiwa ni pamoja na kutoa kero mbalimbali zinazoikabili jiji la Tanga ikiwemo; barabara zinazojengwa chini ya kiwango,taa za barabarani zisizowaka, kukithiri kwa vitendo vya Rushwa katika halmashauri ya jiji la Tanga,Ubadhirifu wa fedha za Mradi wa Tasaf, ucheleweshwaji wa makusudi wa ujenzi wa Hospitali ya wilaya ambayo iliafikiwa ijengwe maeneo ya masiwani jijini Tanga. lakini pia walimuomba mkuu wa Mkoa kumweleza Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete kuchukua hatua za Haraka kuvunja baraza la madiwani la Jiji la Tanga ambalo limekuwa likiwakingia kifua Mkurugenzi asisimamishwe kazi kwani Mkuu wa Mkoa hana mamlaka ya kufanya hivyo.hivyo kutokana na hali hiyo wazee wa jiji la Tanga hawana imani na baraza hilo la madiwani na kuamini labda kuna ushirikiano katika utendaji wa maovu katika halmashauri hiyo.




Pichani aliyevaa Suti nyeusi (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga ambaye alikuwa mgeni rasmi Dk Ibrahimu Msengi akisikiliza kwa makini Risala hiyo ya Wazee wa jiji la Tanga.





Wazee wa kiume wa jiji la Tanga waliamua kumzawadia Mkuu wa Mkoa wa Tanga zawadi ya Kofia ya Barkasheh.



Wazee kwa upande wa kina mama walimawadia Mswala kwa ajili ya kuendeleza Ibada.













SIKU YA UFUNGUZI RASMI WA STUDIO YETU YA AUDIO BAADA YA KUWA KATIKA VIUKARABATI KWA MUDA WA MIEZI 3 !!!

Pichani mimi Pashua na Mido Man mwenye Tshirt ya Man U tukishow love ndani ya Studio muda mfupi baada ya kuifungua rasmi.Studio hii inajulikana kama 2morow recodz iko jijini Tanga maeneo ya Nguvumali.Tunawakaribisha wanamuziki wanaofanya aina zote za Muziki.Pia tunawakaribisha wasanii wenye vipaji kwa ajili ya Lebo.
Picha za Graphics na kipupwe kwa mbali.

Mic ya Voco amabayo ni Condensor.


Full Set ya Guitars pia tunayo.wadau mshindwe wenyewe.



Saturday, June 19, 2010

Hiki ni chumba cha voco room kikiwa na full drums set.
Msanii anayewakilisha kundi letu la mziki linalojulikana kama EASY MEN.anajulikana kama Johnior

Mimi pia ninawakilisha kundi hilo najulikana kama Pashua.na ndio Editor wa Blog hii.


Huyu naye anajulikana kama Mido Man nye pia anawakilisha kundi letu.



Pichani anajulikana kama Kasam naye pia ni muwakilishi wa kundi letu la mziki la Easy men.na pia ni kundi pekee jijini Tanga linalomiliki studio yake yenyewe ya Audio.




Saturday, June 12, 2010

BARABARA YA TANGA - PANGANI YAZIDI KUWA KERO KWA WANANCHI WANAOSAFIRI KUPITIA BARABARA HIYO!!!

Pichani baadhi ya mgari yakiwa yamekwama kufuatia barabara hiyo kuwa mbovu na kusababisha wananchi kupata adha kubwa ya usafiri kwani magari mengi yamekuwa yakishindwa kupita kufuatia matope makubwa yaliyotokana na vifusi vilivyosambazwa katika barabara hiyo baada ya kunyesha mvua kubwa.




Baadhi ya magari mdogo yaliamua kupark kusubiria mana hayawezi kuendelea na safari.








JAMANI MSAADA KWENYE TUTA KWA WATU WA TANGA!!!

Pichani baiskeli hiyo nikiwa nimeipark katika kituo cha Polisi Chumbageni.

Pichani ndio jina la hiyo Baiskeli
Juzi siku ya Ahamisi nilifika Internent Cafe moja katikati ya Jiji la Tanga na kausafiri kangu ka baiskeli ya kukodi ili kuwahi add news.nilipark Baiskeli nje na kuingia ndani.lakini wakati nipo katika harakati za kutafuta park ya kaibaskeli kangu nje ya Cafe walipita vijana wawili waliokuwa wamepakizana kwenye baiskeli yao na wakaelekea mitaa ya mbele.
Sasa wakati nipo ndani naendelea kubrowse mara akaingia kijana yule mmoja wao kati ya wale wawili waliokuwa wamepita kwa nje.alipoingia ndani akamuuliza muhudumu wa Cafe kwamba anamuulizia dada mmoja anaitwa Sauda anafanya kazi za kompyuta.
Sasa mimi baada ya kumuona yule kijana machale yalinicheza nikanyanyuka kidogo kuangalia kausafiri kangu kwa nje nilikokapaki kako salama ile kuangalia nikaona tairi ya kausafiri kangu inaondoka taratibu,basi mimi nikaacha kubrowse haraka sana nikaanza kumfukuzia aliyekuwa anaiba kausafiri kangu.nilipofika nje nilimuona anamalizikia kwenye kona sikuweza kumpata.lakini nilishajua kabisa kwamba kila ilivyo huyu kijana aliyekuwa ndani Cafe akiuliza yule aliyekwiba kausafiri kangu ni yule mwenzake aliyekuwa amempakia kwenye baiskeli kabla ya mimi Kuingia Cafe.basi alipotoka Cafe na kutaka kupanda baiskeli yake aondoke mimi nilimkamata na kuanza kumchapa kidogo aseme yule mwenzie ni nani na anakaa wapi kwa maana mchezo wao wote nilishaustukia.basi baada ya kipondo kidogo alikri yule ni mwenzie ila afahamu anapokaa.mimi nikamwambia sasa nachukua hii baiskeli yako mpaka umfate mwenzio mrudishe ya kwangu na nitakupeni ya kwenu.
sasa karibu kabisa na hiyo Cafe kuna Askari wanaolinda benki ya Exim Bank, nikamwambia twende nikupeleke pale na mimi niiache hii baiskeli yako kwa wale askari ukamfate mwenzio mrudishe baiskeli yangu na niwape ya kwenu.na nikamwambia ukibisha nakupigia kelele za mwizi basi akatii amri,wakati tunaelekea kwa hao askari baada ya kama hatua tano alinipochoka na kutimua mbio na kuniachia Baiskeli yake.
Sasa nilikwenda kituo cha Polisi na kutoa taarifa na kunipatia RB No:TAN/RB/3397/10.na polisi kuniambia niiache hiyo baiskeli kwa siku 3 kama hawakutokea kurudisha ya kwangu nichukue hii iwe mali yangu. lakini hoja ni kwamba hii baiskeli waliyokimbia na kuniachia imeandikwa BLACK FIGHTER No:5 kama inavyoonekana hapo juu.inaonekana ni ya kukodi pia.
Sasa msaada ninaohitaji kama kuna mtu yeyote anayefahamu mahali Tanga hii kuna baiskeli zinakokodishwa zimeandikwa jina hilo hapo juu anipe taarifa ili niweze kufatilia.
Contact zangu zipo hapo juu kwenye profile Picture yangu.
Ahsanteni
Wenu Pashua.

Thursday, June 10, 2010

WAZIRI MKULO ATINGA BUNGENI NA KUWASILISHA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2010-2011 LEO!!

Waziri wa Fedha na Uchumi Mh, Mustapha Mkulo akiwasili katika viwanja vya Bunge na Mkoba wenye Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2010-2011 kabla ya kuiwasilisha jioni ya Leo.
Waziri Mkulo akiwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2010-2011 Bungeni Dodoma Jioni ya Leo.

RAISI JAKAYA KIKWETE AIALIKA TWIGA STARS IKULU LEO!!

Raisi Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya Pamoja na Wachezaji wa Twiga Stars lkulu Leo.
Raisi Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Michezo pamoja na Wachezaji wa Twiga Stars.
Dhumuni la Kuialika Ikulu timu hiyo na viongozi wake ni pamoja na Kuipongeza kufuatia Kufika Fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake zitakazofanyika mwezi September nchini Afrika Kusini.
Pia Raisi ameahidi Kuigharamia timu hiyo katika Msaada wa Chakula,Posho na Nauli katika Kambi yao ya Maandalizi inayotarajia kuanza Mwezi Julai.
Picha kwa Hisani ya Issa Michuzi.

KUNDI JIPYA LA MZIKI LA WANAUME LAJITAMBULISHA RASMI.!!!

Kundi la Wanaume lililotengwa kutoka kundi la TMK wanaume Halisi

Kundi hilo linaundwa na wasanii; Juma Jaz, Rich One,Kaka Man, Mzimu, Daz P na A Man.

TASWIRA YA BANDARI YA JIJI LA TANGA LEO ASUBUHI!!!


Wednesday, June 9, 2010

WADAU KAENI TAYARI KWA MISS TANGA!!!

Picha hii nimeipiga pale maeneo ya Club La vida Loca leo asubuhi.