Tuesday, March 22, 2011
POLENI SANA FAMILIA NA BENDI YA MUZIKI YA 5 STAR MODEN TAARAB KWA MSIBA MKUBWA WA KUONDOKEWA NA WASANII 13 KATIKA AJALI YA GARI HAPO JANA USIKU.!!!
Baadhi ya wasamaria wema waliokuwa kenye foleni ya magari baada ya kutokea kwa ajali ya basi dogo la wasanii wa kundi la 5 STAR Moden Taarab wakichunguza kwa makini iwapo kuna mtu aliyebanwa ama kusahauliwa kuokolewa ama mwili wake kubakia eneo hilo baada ya basi hilo kuparamia lori lililosheheni Mbao lililokuwa limeharibika njiani.katika barabara kuu ya Iringa - Morogoro,eneo la hifadhi ya Taifa ya Wanyama ya Mikumi,karibu na kijiji cha Doma,Wilaya ya Mvomero usiku wa kuamkia leo.
Lori lililoparamiana na basi la wanamuziki wa bendi ya 5 Stars Moden Taarab.
Msanii wa kikundi cha Taarab cha East African Melody,Bi Mwanahawa Ally.akiwa wodini katika Hospitali ya wilaya ya Morogoro leo baada ya kujeruhiwa katika ajali ya basi dogo la wasanii wa Kundi la Five Stars Moden Taarab la jijini Dar es Salaam.
Yeye alikuwa msanii mualikwa katika safari hiyo ya kikazi katika mikoa ya nyanda za juu Kusini.
Blog hii ya EAZYMEN.inatoa pole kwa familia zote zilizopatwa na misiba ikiwa ni pamoja na majeruhi na Bendi nzima ya 5 Stars Moden Taarab.Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi Ameni.!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment