Thursday, January 6, 2011
SERIKALI YAINGILIA KATI MZOZO WA KISIASA ARUSHA !!!
Waziri wa mambo ya ndani Mh Shamsi Vuai Nahodha na Inspecta Jeneral wa Polisi Said Mwema.wakati waziri alipozungumza na waandishi wa habari.
Waziri Shamsi Vuai alisema serikali imeamua kuingilia kati Mgogoro wa kisiasa jijini Arusha na kutaka pande mbili zinazosagana kukaa meza moja na kufanya makubaliano na si vurugu.
Waziri aliyasema haya ikiwa ni siku moja baada ya kutokea vurugu katika mji wa Arusha kufuatia kuvunjwa kwa maandamano ya Chama cha Chadema yaliyokuwa yafanyike jana na kuvunjwa na jeshi la polisi kwa kile ilichoelezwa kuwa maandamano hayo si halali.hata hivyo kufuatia Vurugu hizo imepelekea watu 2 kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa vibaya.
Waziri Shamsi vuai alisema Serikali imeamua kuziweka pande mbili zinazokinzana Arusha ili kuleta Amani na kuiendeleza Arusha.
Aidha pia waziri Nahodha aliyeambatana na Inspekta Jenerali wa Polisi Said Mwema alisema Askari yeyote atakayegundulika kwenda kinyume na mipaka ya kazi atachukuliwa hatua za kisheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment