SIKILIZA NYIMBO ZA EASYMEN HAPA:


Electronic Press Kit
Quantcast

Tazama Small Interview ya Easymen Studio Hapa:

Monday, January 31, 2011

MUUMIN MWINJUMA ARUDI UPYA NA BENDI YAKE YA BWAGAMOYO SOUND !!!


Muumin Mwinjuma kocha wa dunia kama anavyojulikana kwa jina la kimuziki akiimba jukwaani wakati bendi yake ya Bwagamoyo ikiisindikiza African Stars Twanga Pepeta kwenye bonanza lao linalofanyika kila siku za Jumapili katika viwanja vya Leaders Club kinondoni jijini Daresalam.ambapo watu wengi waliojitokeza katika onesho hilo walionekana kuvutiwa na kibwagizo cha ghani zake,Japo kikombe cha chai nataka japo kimo.... kikombe cha kahawa.
Kundi zima la Bwagamoyo Sound likiongozwa na Muumin Mwinjuma kiongozi wa bendi hiyo katika onyesho lao lilifanyika katika viwanja vya Leaders Club.

Wanenguaji wa kundi la Bwagamoyo Sound wakionyesha vitu vyao katika onyesho lao katika viwanja vya Leaders jana Jumapili wakati bendi hiyo ilipoipa kampani bendi Nguli ya African Stars wana Twanga na Kupepeta.

Thursday, January 27, 2011

BABA MZAZI WA BW MISOSI AFARIKI DUNIA !!


Baba Mzazi wa Mwanamuziki wa Bongofleva Joseph Rushau aka BWANA MISOSI Mzee Gabriel Rushau Amefariki Dunia leo asubuhi katika Hospital ya Regency jijini Dar.

Akiongea na blog hii majira wa saa 2 asubuhi Bw Misosi alisema naomba nikujulishe nawe uwajulishe na wengine kwamba baba yangu mzazi amefariki dunia.

Blog hii ya Eazy Men an washkaji wote wa Tanga tunakupa pole kwa msiba huo mkubwa ulioipata familia yako.na tunaiombea familia yenu iwe na uvumilivu katika kipindi hiki kugumu cha msiba mkubwa wa kumpoteza baba yenu mpendwa Mzee Gabriel Rushau.

Mungu Ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na Ina lilah wa ina ilahi rajiun!

Friday, January 21, 2011

LYOD NCHUNGA AZUNGUMZIA MATATIZO YAKE NA WANAYANGA NDANI YA KLABU HIYO.!!!


Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Lyod Nchunga akiongea na wanahabari leo kwenye makao makuu ya klabu hiyo wakati alipotoa tamko la kulaani mkutano ulioitishwa na wanachama wa Yanga jana Klabuni hapo na kumtaka ajiuzulu kwa kukiuka katiba ya Klabu hiyo.
Nchunga amesema mkutano huo ulikuwa batili na ni uvunjaji mkubwa wa katiba ya Yanga lakini akaongeza kwamba watu wana hofu na msimamo wake wa kuamua kufanya ukaguzi wa mahesabu ya klabu hiyo kitu ambacho kinawatisha watu ambao wamekuwa wakitumia vibaya fedha za klabu hiyo.
Kikao hicho kilimtuhumu Nchunga kwamba amemuandikia barua Ndg Francis Kifukwe ili aandae mchakato wa kampuni ya biashara ambayo itaanza kuuza vifaa vya michezo vya Klabu hiyo. Lyod amekiri kukiuka utaratibu kwa kuandika barua hiyo na amesema hajapokea barua yeyote ya kumpa adhabu lakini kama watamuandikia barua hiyo ataipokea na kujua hatua gani atachukua.
Aliyepo Kulia katika picha ni Katibu mkuu wa Klabu ya Yanga Lawrence Mwalusako.

KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM !!!


Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi, Rais Jakaya Kikwete akiendesha kikao cha kamati kuu ya chama hicho kilichofanyika jana Ikulu jijini Daresalaam.(PICHA NA RAMADHANI OTHMAN)

Makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar,Rais mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume na Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi na Mjumbe wa NEC,Dr Ali Mohamed Shein wakifurahia jambo katika ukumbi wa mkutano wa kikao cha kamati kuu ya chama hicho huko Ikulu jijini Dar es Salaam jana.

KUTANA NA MDAU BENEDICT KAGUO !!


Pichani ni mdau wa Blog hii Bw Benedict Kaguo ambaye ni Redio Presenter wa Redio ya MWAMBAO FM (Sauti ya Tanga) na pia ni muandishi.

Thursday, January 6, 2011

SERIKALI YAINGILIA KATI MZOZO WA KISIASA ARUSHA !!!


Waziri wa mambo ya ndani Mh Shamsi Vuai Nahodha na Inspecta Jeneral wa Polisi Said Mwema.wakati waziri alipozungumza na waandishi wa habari.
Waziri Shamsi Vuai alisema serikali imeamua kuingilia kati Mgogoro wa kisiasa jijini Arusha na kutaka pande mbili zinazosagana kukaa meza moja na kufanya makubaliano na si vurugu.
Waziri aliyasema haya ikiwa ni siku moja baada ya kutokea vurugu katika mji wa Arusha kufuatia kuvunjwa kwa maandamano ya Chama cha Chadema yaliyokuwa yafanyike jana na kuvunjwa na jeshi la polisi kwa kile ilichoelezwa kuwa maandamano hayo si halali.hata hivyo kufuatia Vurugu hizo imepelekea watu 2 kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa vibaya.
Waziri Shamsi vuai alisema Serikali imeamua kuziweka pande mbili zinazokinzana Arusha ili kuleta Amani na kuiendeleza Arusha.
Aidha pia waziri Nahodha aliyeambatana na Inspekta Jenerali wa Polisi Said Mwema alisema Askari yeyote atakayegundulika kwenda kinyume na mipaka ya kazi atachukuliwa hatua za kisheria.

Wednesday, January 5, 2011

KUFUATIA MAANDAMANO YA CHADEMA YALIYOVUNJWA NA POLISI LEO JIJINI ARUSHA NA KULETA VURUGU VIONGOZI WA CHADEMA WATIWA MBARONI !!


Viongozi wa Chadema katika maandamano leo kabla ya kutawanywa na polisi na wengine kutiwa mbaroni.

Maandamano ya wanaosadikiwa kuwa ni wanachama na wapenzi wa Chadema yakikatisha mitaa ya Arusha.

Maandamano yakiwa yamepigwa Stop.

Polisi wakiyapiga Stop maandamano hayo.

Baadhi ya maeneo ya katikati ya Jiji la Arusha palikuwa hapatoshi.
Habari zaidi zinadai kwamba watu kadhaa walijeruhiwa katika vurugu zilitokea katika maandamano hayo.Pia imeelezwa kwamba Viongozi wa juu wa Chama cha Chadema akiwemo mwenyekiti,Freeman Mbowe, Katibu mkuu,Dr Wilbroad Slaa, Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Mh Lema na Mbunge wa Moshi mjini,Mzee Ndesamburo wanashikiliwa na Jeshi la polisi kwa madai wao ndio chanzo cha kutokea kwa vurugu hizo za leo.
Mungu ibariki Arusha, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika,Amen.