Wednesday, November 3, 2010
SAMWEL SITTA ACHUKUA TENA FOMU KUTETEA KITI CHAKE CHA USPIKA BUNGE LIJALO !!!
Spika anayemaliza mda wake Mhe. Samuel Sitta leo amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika wa Bunge katika Bunge la Kumi kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema wiki ijayo mjini Dodoma.
Spika Sitta amechukua fomu hiyo kupitia chama chake cha CCM katika ofisi ndogo za CCM Lumumba, Dar es Salaam na kuijaza kisha kuirudisha leo hii baada ya kukamilisha mahitaji yote ikiwa ni pamoja na kugharamia fomu hiyo kwa kiasi cha Tsh 500,000/= kwa mujibu wa taratibu wa chama hicho.
kwa Mujibu wa ibara ya 84 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, chama chochote cha siasa kilichosajiliwa kina haki ya kushiriki katika Uchaguzi wa Spika kwa kumpendekeza mwananchama wake mmoja ambaye ni Mbunge au asiye Mbunge mwenye sifa za kuwa Mbunge kuwa Mgombea wa nafasi hiyo.
Katika picha juu Spika anayemaliza muda wake Mhe. Samuel Sitta akisaini kitabu cha watu waliochukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika kwenye Ofisi za CCM Lumumba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment