Ni ngumu kuamini kama rafiki na kaka yetu mpendwa Abbel Motika umetutoka duniani. lakini ukweli ni kwamba kweli Mr Ebbo ametutoka duniani.
Leo asubuhi saa 12 asubuhi nilipata simu kwamba Mr Ebbo amefariki dunia.sikuweza kuamini hadi nilipoamua kufunga safari milango ya saa 4 asubuhi nyumbani kwa wazazi wake maeneo ya Kisosora jijini Tanga, Nilipofika nyumbani kwa Mzee Motika ambaye ndie baba mzazi wa Mr Ebbo nilianza kuamini baada ya kuona watu wengi kidogo na magari na pikipiki. nilijitahidi kumpata baba mzazi wa Mr Ebbo mzee Motika na akanihakikishia kweli mwanae Abbel Motika maarufu kama Mr Ebbo ambaye amewahi kuwika katika tasnia ya Muziki wa bongofleva na vibao mbalimbali kama Mimi Mmasai na Kamongo kwamba amefariki dunia jana alfajiri jijini Arusha alikokuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda kidogo.
Kuhusu taratibu za mazishi Mzee Motika alinieleza kwamba Mazishi ya mtoto wake Abbel Motika maarufu kama Mr Ebbo yatafanyika jijini Arusha siku ya Jumatatu na msiba utakuwa nyumbani kwao Arusha karibu na Club Masai Camp. Misa ya kumombea marehemu itaanza Jumatatu saa 7 mchana.
Pia nilibahatika kuongea na marafiki wenzangu ambao Mr Ebbo alikuwa rafiki yetu wa karibu kama, Jeff maarufu kama Jeff Production, Msanii wa bongofleva Ruwa,na Ben Naburi nao walionyeshwa kushtushwa na taarifa hizi kwa sababu hali ya ugonjwa wa Mr Ebbo haikuwa siriasi kiasi hicho,
Kutoka kwa marafiki wa jijini Tanga, taratibu za kusafiri kwenda kwenye mazishi ya kijana mpendwa wetu zimeandaliwa na marafiki wote wanaohitaji kwenda kwenye msiba huu wafike nyumbani kwa wazazi wa Mr Ebbo au wawasiliane na Jeff Production au Ben Naburi. safari ya kuelekea kwenye msiba kwa marafiki wa marehemu itafanyika siku ya Jumatatu saa 10 alfajiri ili kuwahi misa inayotazamiwa kuanza majira ya saa 7 mchana jijini Arusha.
Blog hii ya Easymen inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote bila kuwasahau mashabiki zake wote wa muziki wake kokote walipo duniani. Mungu ilaze roho ya marehemu Abbel Roshoroo Motika mahala pema peponi
AMINA.