SIKILIZA NYIMBO ZA EASYMEN HAPA:


Electronic Press Kit
Quantcast

Tazama Small Interview ya Easymen Studio Hapa:

Saturday, August 28, 2010

MH,,SIJUI NI KWELI AU SI KWELI !!!

CHAMA CHA CUF CHAANZA KAMPENI ZA UBUNGE JIJINI TANGA !!!


Mgombea Ubunge wa jimbo la Tanga Mjini kupitia tiketi ya Chama cha CUF,Mh Mussa Bakari Mbaruku.

Hapa akiwa jukwaani akiwahutubia wananchi wa Mabawa jijini Tanga katika viwanja vya Tropicana.


Wananch mbalimbali walijitokeza kusikiliza kampeni za mgombea huyu.

Wednesday, August 25, 2010

KAZI KWETU WANANCHI !!!


TBL YAJITOSA KUDHAMINI BONGO STAR SEARCH KWA MIAKA 3 !!!


Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akitangaza udhamini miaka mitatu wa shindano la Bongo Star Search katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya Paradise jijini Dar es Salaam leo mchana. Kulia ni Mkurugenzi wa Benchmark Production, Ritta Paulsen.

Mkurugenzi wa BenchMark Production,Madame Ritha Paulsen akiongea leo katika ukumbi wa hoteli ya Paradise uliopo ndani ya jengo la Benjamin Mkapa wakati wa utambulisho wa mdhamini mkuu mpya wa Bongo Star Search ambaye ni kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chak cha Kilimanjaro premium lager.kushoto ni Meneja wa bia ya Kilimanjaro,George Kavishe na kulia ni Afisa masoko na mafunzo wa TBL,Edith Bebwa.


Bongo star search ni moja ya kipindi kinacho rushwa na television hapa nchini Tanzania ambacho kime fanikiwa kwa kiwango kikubwa kabisa kuinua vipaji vya wanamuziki wa Tanzania.

Ikumbukwe kuwa mwaka jana kampuni ya kutengeneza bia hapa nchini TBL kwa kupitia kinywaji chake kinachojihusisha na maswala ya muziki Kilimanjaro premium lager. Ilishiriki kama mmoja wa wadhamini wa shindano hilo.

Uhusiano huu mkubwa wa kampuni hizi mbili umetokana na sababu kuu kwamba BSS inahusika kutafuta na kuinua vipaji vya wanamuziki hasa vijana wa umri wowote ambapo Kilimanjaro premium lager kufuatia kauli mbiu yake ya Kufikisha Muziki wa Tanzania Kilele cha mafanikio kwa upande mwingine ina husika na muziki wa vijana wa Kitanzania.

Kilimanjaro premium lager imekua ikunga mkono juhudi za kuendeleza Muziki hapa Tanzania kwa kiwango cha juu.. Ikiwa mdhamini mkubwa kwenye zoezi la kutoa Tunzo za Muziki Tanzania kila mwaka,Tunzo zinazojulikana kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards. Ndio maana Kilimanjaro premium lager imeona hakuna sababu ya wao kutoshirikiana na BSS 2010 katika kuinua vipaji vya wanamuziki wa Tanzania.

Kilimanjaro premium lager imeandikisha mkataba wa kuwa mdhamini wa Bongo star search kwa kipindi cha miaka mitatu ambayo ni BSS 2010, BSS 2011, BSS 2012.

Washiriki wa BSS watashirikishwa katika mambo mbali mbali yakiwemo mashindano yatakayo kua yanafanyika siku hadi siku katika jumba la BSS KILI HOUSE 2010.

BSS 2010 itakuwa ikirusha hewani kila jumapili saa tatu na robo usiku (3:15) kupitia television ya ITV ikishirikiana na Radio one na magazeti ya The Guardian ,Nipashe.
unatakia kufuatilia shindano hilo bila kukosa na pia ni muhimu kupiga kura yako ili kuweza kuwachagua watakao weza kushiriki mpaka mwisho .

shiriki nasi ili kuweza kukamilisha ndoto za wanamuziki wetu.

MWANADADA DORA TEMU AJISHINDIA ML 100 ZA JIKOKI NA TIGO !!!


Ofisa Uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando (kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya sh milioni mia moja kwa mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni ya Jikoki, Dora Temu jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Humudi Abdulhussein.

DUH,HII IMEKAA VIPI JAMANI !!!



Kazi kweli kweli...

Monday, August 16, 2010

KIOTA CHA MALAZI NA VINYWAJI NDANI YA JIJI LA TANGA KINAJULIKANA KAMA CENTRAL CITY HOTEL !!!
















WIKI HII NILIPATA MWALIKO WA KUTEMBELEA MAGOROTO HILL IN AMANI !!!!


Mimi na Devi Rasta tukishow love.

Punde tu baada ya kufika Magoroto sehemu inayotarajiwa kuwa kivutio cha watalii hivi punde.

Devi Rasta mmiliki wa Kampuni ya Utalii ya ILYA TOURS akishow love ndani ya Camera ya Easymen.

Laurent ambaye pia ni katibu wa Taasisi ya kukuza na kutangaza Utalii mkoa wa Tanga(TATONA)akishow love ndani ya camera ya Easymen.

Sehemu mojawapo ya vivutio vilivyopo Magoroto.

Barabara za huku bwana zinatia uvivu yani ukitizama chini unaona ulipotoka.

Msafara wa magari yaliyotupeleka kwenye tour hii.

Washiriki wa tour hii wakitembea kwa miguu kuangalia vivutio vya sehemu hii.

Friday, August 13, 2010

VACATION PASHUA NA AHMED NDANI YA ZENJI !!


Wadau Pashua na Ahmedi wakishow love ndani ya Boat.

Ndani ya Forodhani @ night

Mdau Pashua na rafiki Mwindadi ndani ya Forodhani.


















Saturday, August 7, 2010

LADY JAYDEE AFUNIKA MZALENDO PUB JANA KATIKA KUAZIMISHA MIAKA 10 KATIKA GEMU !!!


Lady jaydee akiwa jukwaani akifanya makamuzi na wanamuziki wenzie wa Machozi Band

Lady Jaydee akikata keki kuashiria kutimiza miaka 10 tangu aingie katika tasnia ya Muziki rasmi.Hongera sana Binti Machozi.


Mashabiki lukuki walijitokeza kumpa sapoti Binti Machozi na kukongwa roho zao vilivyo.