SIKILIZA NYIMBO ZA EASYMEN HAPA:


Electronic Press Kit
Quantcast

Tazama Small Interview ya Easymen Studio Hapa:

Thursday, September 30, 2010

MWANAMUZIKI CHEGE CHIGUNDA ACHAGULIWA KUWANIA TUZO ZA ZUMARI !!!


Have been nominated for Nzumari Awards in the category of Best Male Artist,
the Ceremony wil b on 9
th oct@Club seafront Mombasa,
don't miss!

Wednesday, September 22, 2010

MWAKALEBELA ATIKISA IRINGA.AKUBALI YAISHE NA KUYAZIKA MAKUNDI !!


Mgombea Urais wa chama cha CCM,Mh Jakaya Kikwete akiwa na Frederick Mwakalebela kwa pamoja wakiwasalimia wananchi waliofika kwenye mkutano wa kampeni za chama hicho uliofanyika leo mjini Iringa

Wwwoooowww..!

Mgombea Urais chama cha CCM,Mh Jakaya Kikwete na Frederick Mwakalebela.

================


Frederick Mwakalebela ashangiliwa kuliko mgombea urais wa CCM, jazba ya wana Iringa dhidi ya kutemwa kwa kwake yaonyeshwa mbele ya Jakaya Kikwete, yeye aamua kupanda naye jukwaani .




Hata hivyo CCM jimbo la Iringa mjini imeweza kutumia jukwaa hilo la mgombea Urais kwa kuwataka wagombea wote walioshiriki katika kinyang’anyiro cha kura za maoni kupanda jukwaani ili kuvunja makundi huku wote wakikosa kushangiliwa zaidi ya Mwakalebela aliyeonyesha kushangiliwa kwa nguvu zote kuliko hata burudani zilizokuwepo hapo na wagombea wenzake.





Akitangaza kuvunja makundi ya kura za maoni Mwakalebela alisema kuwa kwa sasa ataelekeza nguvu zake zote kwa Mbega kama mgombea ubunge wa jimbo hilo na madiwani wote wa CCM na mgombea huyu wa urais Dr.Kikwete na kuwataka wapinzani wasimtumie kama sera zao.Picha zote kwa hisani ya Francis Godwin kutoka Iringa.

Tuesday, September 21, 2010

Sunday, September 12, 2010

GENEVIEV EMANUEL NDIYE MISS TANZANIA 2010 !!!


Ni furaha na tabasamu ya kutosha kabisa kutoka kwa binti Geneviev Emanuel pichani kutoka kitongoji cha Temeke,ambaye ndiye aliyelinyakua taji la Miss Tanzania 2010 usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City,Mwenge jijini Dar na kuhudhuriwa na watu kibao,aidha mshindi wa pili alikuwa ni mrembo kutoka Arusha Glory Mwanga na mshindi wa tatu kutoka kitongoji cha Ilala,mrembo Consolata Lukosi.

Saturday, September 11, 2010

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA MECHI YA SIMBA NA AZAM FC LEO KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI JIJINI TANGA,AMBAPO SIMBA ILITOKA KIFUA MBELE KWA MABAO 2 - 1!!!


Kocha Mkuu wa Timu ya Simba Phiri akishow love kwa mashabiki wakati wa kuondoka uwanjani

Kocha wa Timu ya Taifa Jan Paulsen akiwa kwenye iliyomleta uwanjani pamoja na Afisa habari wa TFF Florian Kaijage.

K ocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania Jan Paulsen akishow Love ndani ya Kamera ya blog hii ya Easymen ndani ya Uwanja wa Mkwakwani.

Afisa habari wa TFF Florian Kaijage akiondoka uwanjani baada ya Mchezo baina ya Simba na Azam kuisha.

Basi la Wachezaji wa Azam Fc likiwa limepark tayari kwa safari ya kurudi Dar es Salaam baaday ya mchezo wao na Simba katika Hotel ya Central City barabara 8 jijini Tanga ambapo ndipo wachezaji hao walipofikia.

Mashabiki wa Timu ya Simba wa jijini Tanga wakimpa hongera mtoto wa Home Uhuru Suleiman akiwa kwenye gari baada ya Mechi kumalizika.

Mchezaji wa Simba akishow love na mashabiki wa Timu hiyo wakati wakitoka Uwanjani.

Basi la wachezaji wa Timu ya Azam Ndani ya Uwanja wa Mkwakwani punde tu baada ya Mechi kumalizika na Simba kutoka kifua mbele kwa Goli 2 - 1.

Basi la mashabiki wa Simba toka Dar es salaam likiondoka ndani ya Uwanja wa Mkwakwani kwa mbwembwe baada ya kupata ushindi dhidi ya Azam Fc.

Baadhi ya Mashabiki waliamua Kuingia uwanjani kupitia ukutani kutokana na Ticket za Mchezo huo kuisha mapema na uwanja kujaa na Kufungwa mida ya Saa kumi na nusu jioni.

Hii pia ilikuwa ni njia ya Kuingia uwanjani baada ya kuwa Ticket zimekwisha mapema na uwanja kufungwa.amabpo inasemekana Ticket zilitengenezwa 14,000 zote ziliisha.

Baadhi ya Mashabiki wa Azam waliotoka Dar es Salaam wakifanya vurugu mlango mkuu wa Uwanja wa Mkwakwani baada ya kuambiwa kuwa Ticket zimekwisha na hawataweza kuingia na kuona mchezo huo.
Mashabiki wengi waliotoka mikoani na wa jijini Tanga hawakuweza kuona mchezo huu kutokana na Ticket kuwa kidogo na Uwanja kujaa.hata mimi mwandishi wa Blog hii nilifika Uwanjani Saa kumi na dakika tano pamoja rafiki zangu lakini hatukuweza kuingia na kuona mchezo huu.

DALADALA LAGOMA KUENDELEA NA SAFARI NA KUPARK KATIKATI YA BARABARA BAADA YA KUHARIBIKA!!!


Leo katika pitapita zangu mitaa ya Mabawa jijini Tanga nilikuta daladala hili likiwa limekataa kuendelea na safari baada ya kukatika Timing Road.
a href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjTGGqz83gkr0i5fP00LW3tfMOnO8py9Evt00l6mKBQntom40SPlaiDEMazeVyX1HpmzAYfRG3X31t9_mvpceqoHmhilBuh3fyEAoHX-x86fOwYNbuoBbbRlZLro-1iaad_8LJod4q_QIM/s1600/Kwikwi+2..JPG">
Daladala hilo likiwa katikati ya Barabara.je nani wa kuchunguza kama chombo cha moto nia salama kwa kuingia barabarani ni dereva au Tajiri ?????.hii ni Hatari sana kama daladala hili lingekuwa katika mwendo kasi.

Friday, September 10, 2010

MGOMBEA URAIS WA CCM DR JAKAYA KIKWETE ATOA MKONO WA EIDD KWA WAISLAM MKOANI TANGA!!


Mgombea Urais kwa chama cha CCM,Mh Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu muda mfupi baada ya kumalizika kwa swalla ya Iddi iliyoswaliwa katika Msikiti Mkuu wa Riyadh mjini Tanga leo asubuhi

Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Mufti Mkuu sheikh Issa Shaaban Simba wakati wa Swalla ya Iddi iliyoswaliwa mjini Tanga leo.Katikati anayeangalia ni Mgombea Urais kwa chama cha CCM,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete

Mgombea Urais kwa chama CCM,Mh Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono wa Iddi na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi wakati wa Swalla ya Iddi iliyoswaliwa katika Msikiti mkuu wa Riyadh mjini Tanga.Mzee Mwinyi ndiye mgeni Rasmi katika baraza la Iddi litakalofanyika kitaifa mjini Tanga.

Mgombea Urais kwa chama cha CCM,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaaban Simba wakati wa swalla ya Idd iliyoswaliwa kwenye Msikiti Mkuu wa Riyadh mjini Tanga leo asubuhi (picha na Freddy Maro)

Tuesday, September 7, 2010

HATIMAE KEISHA AZUNGUMZIA KILICHOMTOA TIPTOP CONNECTION



First Lady wa TIP TOP CONNECTION Keisha akiwa katika picha ya pamoja na wenzake.

**************

Kwanza ni ngumu mimi kufukuzwa Tip Top kwa sababu uwezo wangu unafahamika dhahiri, ukweli ni kwamba nikitoka basi kundi litayumba sana, mchango wangu ni mkubwa kimuziki. Mimi nimejitoa na sababu kubwa ni kwamba sina imani na uongozi,”

“Babu Tale asiseme uongo na kama wanahitaji nirudi, kabla ya yote nilipwe pesa zangu 480,000 ambazo ni madeni ya pesa alizokuwa akinisainia baada ya shoo na kuniletea pungufu, mwisho siwezi kulumbana nao kwa sababu nina mambo mengi ya kufanya kwa ajili ya kuongeza uchumi wa taifa letu,”

WOTE TUTAKWENDA NA TUTAFIKA SALAMA,TEH TEH ...!!!!!