SIKILIZA NYIMBO ZA EASYMEN HAPA:


Electronic Press Kit
Quantcast

Tazama Small Interview ya Easymen Studio Hapa:

Friday, April 30, 2010

WAZIRI KAPUYA ATANGAZA VIMA VYA CHINI VYA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Prof. Juma Kapuya (shoto) akitangaza viwango vipya vya mishahara kwa kima cha chini kwa wafanyakazi wa sekta binafsi leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Viwango hivyo vya kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi vinazigusa sekta za Afya,Huduma za Kilimo, Viwanda na Biashara, Mawasiliano, Sekta ya Madini, Bandari na sekta ya Uvuvi, Wafanyakazi wa majumbani,sekta ya ulinzi Binafsi na Hoteli. Habari na Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

Ufafanuzi wa viwango hivyo.
1. Huduma za Afya - Tshs 80,000/=

2.Sekta ya Kilimo - Tshs 70,000/=

3.Viwanda na Biashara - Tsh. 80,000/=

4. Usafirishaji na Mawasiliano
-Huduma za anga 350,000/=
- Clearing and Fowarding 230,000/=
- Mawasiliano ya Simu 300,000/=
- Usafiri wa nchi kavu 150,000/=

5.Madini - Migodini 350,000/=
- Wachimbaji wadogo -150,000/=
- Wauzaji wadogo na watoa leseni 250,000/=
- Brokers Licenses 150,000/=

6. Maji (Bahari na Uvuvi) - Tsh. 165,000/=

7.Majumbani:
- Majumbani (mabalozi na wafanyabiashara wakubwa)- isiwe chini ya Tsh 90,000/=
- Maafisa wenye sitahili ya kulipiwa huduma hii -isiwe chini ya Tsh.80,000/=
- Wengineo - Tshs 65,000/=

Mahotelini:
- Hoteli kubwa za kitalii - 150,000/=
- Hoteli za kati - 100,000/=
- Hoteli ndogondogo,mabaa, nyumba za wageni na migahawa- 80,000/=

8. Ulinzi Binafsi.
-Makampuni makubwa na makampuni ya kigeni - 105,000/=
- Makampuni mengineyo- 80,000/=


9. Sekta nyingine ambazo hazikutajwa - 80,000/=

PRESIDENT KIKWETE ARIVES IN KAMPALA FOR THE EAST AFRICA INVESTMENT CONFERENCE!!

A young ugandan girl Clarissa Kanyenjeka presents a bouquet of flowers to president Jakaya Kikwete shortly after he arrived at Entebbe International Airport for the EAC investment conference to be held to Munyonyo Speke Resort in Kampala.

Wednesday, April 28, 2010

POLENI SANA NDUGU ZETU WA CHUO CHA KIISLAM CHA SHAMSIL MAARIF KWA MSIBA MKUBWA MLIOUPATA SIKU YA JANA.

Blog hii ya EASY MEN kutoka Nguvumali jijini Tanga.inatoa pole kwa Chuo cha kiislam cha Shamsil Maarif cha jijini Tanga.kwa kupata msiba mkubwa wa wanafunzi uliotokana na ajali iliyotokea siku ya jana jumanne 27/04/2010.majira ya Saa 5 Usiku maeneo ya mabanda ya papa jijini.na kusababisha vifo vya wanafunzi takribani 19.

Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi

AMENI.

Kumradhi wadau kwa kukosa picha.

BADO SIKU 2 TU KUSHUHUDIA MISS CHUMBAGENI WADAU!! HAPATOSHI


Saturday, April 24, 2010

C PWAA ANAOMBA KURA ZENU WADAU!!

Habari za kazi ndugu, mashabiki na marafiki zangu. Poleni kwa majukumu. Kijana wenu nimepata nafasi ya kuchaguliwa kushiriki kwenye tunzo za muziki mbalimbali Tanzania mwaka huu 2010. Naomba unipigie kura kwa kutumia maelekezo haya:TUNZO ZA KILIMANJARO ( KILI MUSIC AWARD) 2010 :VIDEO BORA YA MWAKATuma neno KILI T13 kwenda 15723Au piga kura online, tembelea:

http://www.kilitime.co.tz/awards/2009/nominees_2007.php?Nenda chini ya page,tafuta Video bora ya muziki ya mwaka..tiki Problem-Cpwa kisha weka email yako na bofya VOTE.TUNZO ZA XXL ( XXL TEEN AWARDS) 2010Video Kali ya mwaka: Tuma neno TN F3 kwenda namba 15551Video kali ya kucheza : Tuma neno TN E3 kwenda namba 15551Mrembo wa mwaka kwenye Video:Tuma neno TN C1 kwenda 15551Au piga kura online, tembelea:www.nipe5.com

Kama huifahamu video ya Problem bofya hapa:http://www.youtube.com/watch?v=OXhqQY4QxvE&feature=related

Asanteni sana.Pwaaaa!

Sunday, April 18, 2010

KAMPUNI YA SIMU YA ZAIN YAMWAGA MSAADA WA VITABU WILAYA YA LUSHOTO,TANGA.

Mkuu wa wilaya ya Lushoto Sophia Mjema (katikati) akimkabidhi Juma kibwana mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Vugabazo iliyopo wilayani humo wiki hii. Vitabu vyenye thamani ya Shilingi milioni 2 ambavyo vimetolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain kupitia mradi wake wa “Build Our Nation”. Kwa ajili ya shule hiyo ya Vugabazo na shule ya sekondari ya Kisaba mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Zain, Muganyizi Mutta.
Mkuuu wa wilaya ya Lushoto Sophia Mjema (katikati) akimkabidhi Frank Glibety mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Kisaba iliyopo wilayani humo vitabu vyenye thamani ya Shilingi milioni 2 ambavyo vimetolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain kupitia mradi wake wa “Build Our Nation”. Kwa ajili ya shule hiyo ya Kisaba na shule ya sekondari ya Vugabazo mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Zain, Muganyizi Mutta.


Saturday, April 17, 2010

HAYA WATANI MAMBO NI HAPO KESHO 16:30


AY ASHINDA TUZO ZA TENEEZ 2010 NCHINI KENYA,AWA MSANII BORA WA AFRIKA MASHARIKI 2010.

Ay au Ambwene Yesaya.mwanamuziki wa Bongo flava ametunukiwa tuzo ya Msanii bora wa Africa Mashariki nchini Kenya leo.katika tuzo zinazojulikana kama TENEEZ Award.Hongera na Bongo oye!!

TUSHEE KIDOGO PICHA HII YA HARUSI YA MWANAMUZIKI QJAY,ILIYOFANYIKA JUZI.

Mmmh hapa bwana alitulia.unaweza kusema sio yule ambae akiwa jukwaani kashika Mic na vituko vingi.Ni msanii kutoka kundi la mziki la wakali kwanza linaloundwa na yeye Qjay na Makamua.Hongera sana!!

KUELEKEA MTANANGE WA WATANI WA JADI.MASHABIKI HOOOOF !!!!

Kazi kweli kweli.usihofu ushindi utaelekea msimbazi.ila sijakuelewa hapo unasali au unawaza!!

TUKAE TAYARI KWA MKAO WA KUJUA NANI ATAWAKILISHA PANGANI.


WADAU SORY KWA KUTOKUWA UP TO DATE KWA SIKU 6.NILIKUWA MGONJWA WA MALARIA.

Monday, April 12, 2010

TUSHEE VIMATUKIO VYA WEEKEND WADAU!!

Hapa kidogo nikiwa kwenye kufanya interview na hawa watu.
Nikiwa katika shavu la Surprise Birthday ya rafiki.viugonjwa vyetu vya kekiz vilikuwepo.

Sunday, April 11, 2010

MTOTO WA KWETU ANAOMBA KURA ZETU WADAU!!


Hi ndugu

Kwenye Kili Music Awards naomba unipigie kura yako kwa wimbo bora wa ragga - MUNGU YUKO BIZE.Kupiga kura andika Kili M56 na unatuma kwenda namba 15723.
Piga kila siku uwezavyo ili niweze kunyakuwa tuzo.

Saturday, April 10, 2010

HEMEDI (PHD)SASA KUDEAL NA MZIKI TU.

Msanii wa mziki wa bongo fleva kutoka Pande za Mkoa wetu wa Tanga,Hemedi PHD.amesema kuanzia sasa anaweka kando kujishughulisha na mambo ya Filamu na badala yake ataweka nguvu zake zote kwenye mziki ambao anaamini bado hajautumikia hata robo kutokana na Mafunzo aliyoyapata akiwa Tusker Project Fame.

Friday, April 9, 2010

SUPER STAR 2 WAKIKUTANA

Masupar Star wawili wa Bongo wakiteta jambo.vijana hawa wawili wamefanikiwa sana katika tathnia ya Sanaa.

LIYUMBA AFUTIWA SHITAKA NA MAHAKAMA!!


Friday, April 9, 2010


Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba aliyekuwa akikabiliwa na mashitaka mawili, kutumia vibaya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Shilingi bilioni 221 leo ameondolewa shitaka la kutumia vibaya madaraka na hivyo kubaki na kosa moja.Liyumba aliyekuwa akikabiliwa na kesi hiyo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, alifutiwa shitaka hilo baada ya mawakili wa upande wa utetezi kutoa vielelezo vilivyothibitisha kuwa mteja wao hakuwa na kesi ya kujibu.Mshitakiwa huyo amerudishwa Keko mpaka Aprili 22 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo.

TID na ALI KIBA PERFOMING NDANI YA READING!!

Wasanii wawili kutoka Tanzania TID na ALY KIBA watafanya show ya pamoja tarehe 2 May.katika mji wa Reading nchini England.

MJUE NABII TITO ANAYESEMA POMBE NI DAWA YA MAGONJWA MBALIMBALI




Pichani ni Nabii Tito akiwa katika mahojiano na Star wa Movie za Bongo Vicent Kigosi (Ray)pamoja na kipeperushi chake kinachoelekeza aina za bia zinavyoponya magonjwa mbalimbali.duh hii imekawa sawa wadau.!!!


Thursday, April 8, 2010

Hapo je!!!!

Nadhani hapo Kaujumbe kamefika.teh teh teh........

Wednesday, April 7, 2010

Mchizi na Fisi wake shwarii

Mchizi akikatiza mitaa flani huku akiwa na Mbwa mwitu (Fisi) bila wasi wasi wowote.
duh bongo tambarare.

H BABA kuangusha jiwe jipya soon.



Msanii H Baba anatarajia Kuachia Video mpya itakayoonekana katika Vituo mbalimbali vya Televisheni.pia alisema Audio amefanya katika Studio inayokuja kwa kasi ijulikanayo ka SEDUCTIVE Recordz iliyo chini ya Empty Soulz.

Kwa hisani ya Empty Souls.

Witnes aomba kura zenu


Msanii wa Bongo flavor Machachari Witnez.anaomba mumpigie kura ili aweze kubaki katika shindano la Selebuka linalorushwa hewani kila Jumapili saa 3 Usiku katika kituo cha Televison cha TBC.

Easy Men ndani ya Ta Tv.

Wasanii wanaounda kundi la Mziki wa Bongo flavour la jijini Tanga lijulikanalo kama Easy Men wakishow love ndani ya Studio za Television ya Mkoa wa Tanga.TATV.

Kazi kweli



Mwenzenu nikiumia katika kutimiza majukumu ya kundi.

Shavu la exchange program



Vijana wa Kituo cha vijana Nguvumali jijini Tanga.wakiwa pamoja na vijana wenzao kutoka katika nchi ya Norway.
Kikundi cha Utamaduni cha Jijini Tanga kijulikanacho kama Nguvumali Theatre Group kikiwa kazini kuporomosha burudani.

Easy Men kurelease Chombeza Song


Kundi la Mziki wa Kizazi kipya la jijini Tanga na pia linamiliki Studio ya Audio ijulikanayo kama 2morow Recordz.linatarajia kuachia Ngoma yao ya 5 hewani mwisho wa mwezi huu.
Ngoma hiyo imetengezwa Studio ya 2morow Recordz chini ya Producer Danny.